Jackie Chan kupewa tuzo za heshima za OSCAR

358
0
Share:

Nyota na muigizaji maarufu wa Filamu Duniani Jackie Chan anatarajia kupewa tuzo ya heshima ya Oscar kutokana na sababu mbalimbali akiwa pamoja na nyota wengine watatu. 

Chan mwenye umri wa miaka 62 ambae pia ni mwandishi, muigizaji, muongozaji wa filamu na mkufunzi wa sanaa ya kupigana (martial art) kutoka Nchini China ametajwa kuwa atapewa tuzo hiyo kutokana na mafanikio makubwa aliyoyafanikisha katika tasnia ya filamu. 

Chuo Cha Filamu cha nchini Marekani kilipiga kura katika nafasi hiyo ya tuzo za heshima  kwa Mhariri wa filamu Anne Coates, muongozaji wa waigizaji Lynn Stalmaster na mtenegenezaji wa makala Frederick Wiseman.

Rais wa chuo hicho cha filamu Bwana Cheryl Boone amewataja wanne hao kama waanzilishi na wataalam wenye ujuzi wa utunzi wa hadithi za filamu. 

Chan ambae asili yake ni Hong Kong nchini China amepata umaarufu mkubwa kupitia filamu kadhaa za ngumi na kareti zilizompa mafanikio makubwa maishani mwake 

Ameigiza filamu kama ‘Rumble in the Bronx’ , ‘Rush Hour Franchise’ ‘Who Am I’ ,filamu ya vikatuni maarufu kwa jina la ‘Kung-Fu Panda’,na nyingine nyingi. 

Licha ya mafanikio yake yote Jackie Chan hajawahi kupewa tuzo hizo za heshima za Oscar 

Washindi wengine wa tuzo za heshima ya Oscar pia wanatajwa kuwa wamefanya kazi kwa muda mrefu katika tasnia ya filamu, Anne coates ametumikia tasnia ya filamu kwa kuwa mhariri wa filamu kwa muda wa takribani miaka 60 na ffilamu iliyompa tuzo hizo za heshima ni ‘Lawrence of Arabia’. Lynn Stalmaster anatajwa kushiriki katika utengenezaji wa filamu zaidi ya 200 na Frederick Wiseman amekuwa akitengeneza filamu tangu mwaka 1967.

Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC).

Share:

Leave a reply