Jamii yatajwa kuwa chanzo cha mmomonyoko wa maadili

141
0
Share:

Jamii imetakiwa kusimamia vyema makuzi ya watoto hasa kwa kuwalea katika maadili mema ili Taifa liondokane na visa mbalimbali vya mmomonyoko wa maadili.

Wito huo ulitolewa jana Aprili 14 katika Sherehe ya Maadhimisho ya Siku Kuu ya Utoto Mtakatifu iliyofanywa na Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Polycarp Misugusugu.

Akizungumza katika sherehe hiyo, Paroko Mkuu wa Parokia ya Mt. Polycarp Misugusugu, Father Joseph Kazikunema Mkonde, alitoa rai kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuwalea watoto katika misingi ya dini kama maandiko matakatifu yanavyotuagiza.

Father Mkonde alisema jamii inatakiwa kulea watoto kwenye maadili mema ili kuepusha vitendo vya mmomonyoko wa maadili.

Naye Paroko Msaidizi wa Parokia hiyo, Father Simon Kasimila Shija wakati akiongoza Ibada ya Misa Takatifu, aliwataka watoto hao kudumu katika misingi ya imani kiwemo kujifunza namna ya kuwa watumishi wa kanisa katika umri huo waliokuwa nao ili baadae waje kuwa viongozi bora wa Kanisa Katoliki.

Pia, Father Shija aliwataka watoto hao wasikilize wito wa Upadre na Usister ili waje kuliendeleza kanisa na kazi ya Mungu isonge mbele bila kurudi nyuma.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na watoto kutoka vigango vitatu vya Zogowale, Ngeta na Makazi Mapya, vinavyounda Parokia ya Mtakatifu Polycarp Misugusugu, ambapo wageni rasmi walikuwa Dastan Kalokola na Leticia Kalokola kutoka Parokia ya Wazo.

Naye, Ndugu Kalokola alisema “Tunawashukuru watoto wote pamoja na walezi wao kwa kuweza kufika hapa na kukamilisha tamasha hili pia tuwaomba isi ishiae hapa iwe mwendelezo na tuawaomba walezi muwalee watoto hawa vizuri hili waweze kukua katika misingi ya imani ya kikatoliki.

Na Regina Mkonde

Share:

Leave a reply