Je! Klabu ya Yanga kuishusha Simba Sc leo? Msimamo wa Ligi Kuu ya VPL upo hapa

362
0
Share:

Michezo saba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) inatarajiwa kuchezwa katikati ya wiki hii, kwa leo Machi 8.2016 kuchezwa mchezo mmoja, huku michezo mingine sita ikichezwa kesho siku za Jumatano na Alhamisi katika viwanja mbalimbali nchini.

Mchezo huo wa leo Jumanne, 8 Machi 2016, Klabu ya Yanga (Young Africans)  watakua wenyeji wa Wana Kimanumanu African Sports, mchezo utakaoanza majira ya saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Jumatano Machi 09, 2016 Tanzania Prisons watakua wenyeji wa Kagera Sugar kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, huku Coastal Union wakicheza na ndugu zao maafande wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Mwadui FC watakua wenyeji wa Majimaji katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga, huku JKT Ruvu wakiwakaribisha Toto African katika uwanja wa  Mabatini , Mlandizi mkoa wa Pwani.

Alhamisi Simba SC watawakaribisha Ndanda FC kutoka Mtwara katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku wagonga nyundo wa jiji la Mbeya timu ya Mbeya City wakiwakaribisha Stand United chama la wana katika uwanja wa Sokoine.

vpl22

Michezo inayotarajiwa kuchezwa..

vodacom

Msimamo wa ligi hiyo kabla ya mchezo wa leo, Klabu ya Simba Sc ikiwa ipo kileleni ikiongoza ligi.

Share:

Leave a reply