Jennifer Lopez aachana na mpenzi wake Casper Smart

259
0
Share:

Mwanamuziki wa miondoko ya PoP pamoja na RnB nchini Marekani Mwanadada Jenifer Lopez, ametangaza rasmi kuacha na aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu Casper Smart huku akitoa sababu mbambali kutokana na yeye kufanya hivyo.

Jlo mwenye umri wa miaka 47 ameeleza kuwa haikuwa kazi rahisi mpaka yeye kufikia kutamka hayo ila amekuwa akiishi maisha yasiyo na furaha ndni ya mahusiano yao kwa kipindi kirefu sasa na amekuwa akivumilia ila mwenzake amekuwa sio mtu wa kujirekebisha kila alipokuwa akimwambia.

Mapema wiki iliyopita walionekana pamoja katika ukumbi wa starehe mjini Las Vegas na baadae walielekea katika nyumba ya Lopez bila kuwa na matatizo yeyote yale.

Katika wiki hiyo hiyo siku ya Jumapili, Jlo alienda kumtembelea Marc Anthony ambaye ni mpenzi wake wa zamani na baba wa watoto wake wawili huku wakionekana wenye furaha na kushirikiana vizuri katika sherehe ya kifamilia iliyokuwa ikifanyika nyumbani kwa Marc Anthony na baadae Jlo alipost katika Instagram picha waliyokuwa wamepiga kwa pamoja.

Jenifer Lopez na Marc Anthony walitengana mwaka 2011 na baadae kuwa na mahusiano pamoja na Smart ambaye miaka mitatu baadae waliachana lakini walirudiana tena na kuwa moja kati ya Couple zenye nguvu Zaidi nchini Marekani.

Japokuwa ‘Couple’ hii ilipata dosari mwaka 2014 kwa wawili hao kila mmoja kuishi katika makazi yake, lakini kwa sasa ni moja kati ya mastaa wa walioacha historia katika upande wa Mahusiano kwa kuweza kuongeza orodha ya waliovunja uhusiano wao hivi karibuni.

Casper Smart ni mwigizaji pamoja na mwanamitindo alizaliwa April 6 1987 huko California nchini Marekani ambaye ni mmoja kati ya wanenguaji wa zamani wa Jenifer Lopez.

Na Derick Highiness

Share:

Leave a reply