Jerry Muro apigwa ‘stop’ kujihusisha na soka na kupigwa faini

296
0
Share:

Maneno ambayo alikuwa akiyatoa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro kwa Shirikisho la Soka nchini (TFF) sasa yamemgeukia msemaji huyo baada ya Kamati ya Maadili ya TFF kumkuta na hatia.

Muro amekutwa na hatia ya kuisema vibaya TFF katika vyombo vya habari na hivyo kufungiwa mwaka mmoja kutokujihusisha na soka pamoja na kutakiwa kulipa faini ya shilingi milioni tatu ndani ya siku 90.

Aidha kamati ya maadili ya TFF imetoa nafasi kwa Jerry Muro na TFF kukata rufaa kama watakuwa hawajaridhishwa na maamuzi ambayo yametolewa.

Kwa upande wa Muro amesema kuwa kamati hiyo haijamfanyia jambo sahihi kwani imetoa hukumu ya kesi hiyo akiwa hayupo katika kikao hicho na kutaja sababu ya kushindwa kuhudhuria ni kuwa nje ya kazi kwa kuchukua likizo ambayo amekwenda kupumzika kwao Kilimanjaro.

Share:

Leave a reply