Jeshi la Misri laua wapiganaji 12 wa kundi la IS

108
0
Share:

Vikosi vya Usalama nchini Misri vimewauwa wapiganajaji wa kundi la Dola ya Kiislamu (IS) 12 na kukamata 92 katika mapambano yanayoendelea mjini Sinai.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema leo Jumatatu na Jeshi la Misri, inaeleza kuwa vikosi hivyo pia viliharibu malengo 60 ya wapiganaji hao ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni ya kutokomeza makundi ya waasi wa kiislamu. 

Rais wa Misri, Abdel Fattah Al-asisi anayetarajiwa kuchaguliwa tena katika uchaguzi wa mwezi Machi mwaka huu, mnamo mwezi Novemba, 2017 aliamuru majeshi ya nchi hiyo kuwashinda wapiganaji hao ndani ya miezi mitatu  baada ya kutokea kwa shambuli lililouwa watu zaidi ya 300.

Share:

Leave a reply