Joel Bendera afariki dunia, Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi

509
0
Share:

Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Manyara, Joel Bendera amefariki dunia akipatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Hospital ya taifa Muhimbili Aminieli Aligaesha amesema Bendera alifikishwa hospitalini leo mchana Desemba 6, 2017 akiwa kwenye gari la wagonjwa na ilipofika saa 10:24 jioni wakati madaktari wakiendelea kumpatia matibabu alifariki.

Kufuatia kifo cha Bendera Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi na kueleza kuwa amepokea taarifa hiyo kwa mshtuko.

“Nimepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha Mkuu wa Mkoa Mstaafu Dkt. Joel Nkaya Bendera, natoa pole kwa familia yake na wote walioguswa na msiba huu na pia naungana nao katika kipindi hiki cha majonzi.” amesema Rais Magufuli.

Share:

Leave a reply