Jokate awataka wasanii kusaidia huduma ya afya ya wazazi na watoto

368
0
Share:
Jokate Mwegelo

Mrembo wa Tanzania namba mbili wa 2006, mbunifu mavazi na muigizaji wa filamu za kibongo, Jokate Mwegelo  amewaomba wasanii wenzake na wadau wengine  kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha huduma ya afya ya wazazi na watoto.

Akizungumza mara baada ya kutembelea wodi ya wazazi ya hospitali ya Palestina na kutoa misaada mbalimbali kwa wanawake waliojifungua wakati wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake duniani, Jokate alisema kuwa sekta hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi na kutokana na umuhimu wake, wadau wanatakiwa kusaidia serikali.

Jokate alisema kuwa serikali inafanya kitihada kubwa ya kuboresha sekta  hiyo na kumpongeza Rais Dk John Magufuli kwa kuelekeza nguvu  na kufanikiwa  kutatua  tatizo sugu lililokuwa linaisumbua la  hospitali ya Taifa ya Muhimbili T-scan matatizo kadhaa sugu.

JOK2

Mbunifu wa mavazi, msanii wa filamu na mrembo maarufu nchini, Jokate Mwegelo akikabidhi moja ya msaada wake kwa mmoja wa mama aliyejifungua mtoto wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika hospitali ya Palestina jijini.

“Kila mmoja wetu anajua nini maana ya afya, huwezi kufanya jambo lolote kama huna afya bora, hivyo matibabu bora ni muhimu, serikali inafanya vitu vingi katika kuondoa kero za wananchi wake ikiwemo suala la afya, nimeguswa na kuamua kuunga mkono kupitia kampuni yangu ya Kidoti ambayo inazalisha viatu na nyewe,” alisema Jokate.

Alisema kuwa amefuraishwa na huduma ya wodi ya wazazi ya hospitali ya Palestina na ushirikiano waliopata kuanzia mganga mkuu wa manispaa ya Kinondoni na uongozi wa hospitali hiyo kwa ujumla.

“Kama unavyojua, misaada mingu uelekezwa kwenye hospitali kubwa kubwa tu, kuna hospitali na zahanati nyingi ambazo zinahitaji kusaidia, hivyo wasanii wenzagu, hii ni fursa kwenu kurudisha faida kwa jamii, si lazima utoe fedha, hata kuwaona wagonjwa na kuwafariji,” alisema.

JOK3

Mmoja wa mofisa wa kampuni ya Suining Zerong Commercial Trading, Shuxia B akizungumza kwa niaba ya kampuni hiyo. Kampuni hiyo inafanya kazi pamoja na kampuni ya Kidoti.

Alisema kuwa mikakati yake ni kuona anatembelea na kutoa alichonacho kwa hospitali na vituo vya afya mbalimbali nchini.

Mmoja wa maofisa wa kampuni ya Kidoti, Shuxia Bi kutoka China alisema kuwa ni vizuri jamii hasa wasanii wa muziki, filamu, warembo  na wanamitindo kuunga mkono juhudi za serikali katika kutatua matatizo kwa jamii yenye mahitaji maalum. Shuxia alisema kuwa kupitia chapa ya Kidoti wanaamini watafikia wadau wengi jijini nan je ya mkoa.

  Dakitari Mkuu wa hospitali ya Palestina, Kariamel Wandi aliimpongeza Jokate na kampuni yake kusaidia wodi ya wazazi. “Tumefarijika sana, umeonyesha kuwa unajali, wengi wameshindwa kufanya kama unavyofanya pamoja na kuwa na nafasi hiyo, naomba uwe na moyo huo huo,” alisema Wandi.

Wandi alisema kuwa  Jokate amewasaidia wakati muafaka kwani hadi anakamilisha kutoa misaada mbalimbali, jumla ya watoto  26 walizaliwa katika hospitali hiyo. Kati ya hao, 18 ni wasichana na nane ni wavulana.

JOK4

Jokate Mwegelo ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya na mmoja wa maofisa wa kampuni ya Suining Zerong Commercial Trading, Shuaijie Duan wakikabidhi cheti cha shukrani kwa daktari Mkuu wa hosptiali ya Palestina, Dk  Kariamel Wandi.

Share:

Leave a reply