Jose Mourinho amkataa bosi wake wa zamani, Roman Abramovich

254
0
Share:

Kuelekea mchezo wa EPL kati ya Chelsea ambayo inataraji kuwe mwenyeji wa Manchester United, mchezo utakaopigwa katika kesho jumapili katika dimba la Stamford Bridge, kocha wa Manchester United amezungumza kuhusu mchezo huo.

Mourinho ambaye aliondoka Chelsea msimu uliopita baada ya kupata matokeo ambayo hayakumfurahisha mmiliki, Roman Abramovich na mashabiki wa klabu, amesema anakwenda katika mchezo huo akiwa ameshakua na kilichomtokea Chelsea hakiwezi kumtokea kwa mwaka wake wa kwanza akiwa na Man United.

“Muda umewadia nikiwa nimeshakua, nikiwa meneja imara. Nina hisia imara, sio mtoto. Haiwezi kutokea kwa mwaka wa kwanza katika historia yangu ya kazi ya umeneja,

“Nina furaha kuwa na klabu kubwa kama Manchester United katika maisha yangu ya kazi sio kwa miezi mitatu iliyopita, lakini naweza kusema katika mashindano [Ligi Kuu ya Uingereza] ambayo ndiyo ninayoipenda zaidi,” alisema Mourinho.

Aidha Mourinho alizungumza kuhusu uhusiano wake na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich ambaye amewahi kuwa bosi wake wakati akifundisha Chelsea na kusema kuwa hakuwa rafiki yake na wala hakuwa mtu wake wa karibu.

“Ni uhusiano wa mmiliki na meneja, tuliheshimiana sana. Hakuwahi kuwa rafiki yangu, na wala hatukuwa na ukaribu baina yetu,” alisema Mourinho.

Share:

Leave a reply