JPM amwalika Rais wa Zambia kufanya ziara ya siku tatu nchini

731
0
Share:

Rais John Pombe Magufuli amemwalika Rais wa Jamhuri ya Zambia, Edgar Lungu kufanya ziara ya siku tatu nchini kuanzia Novemba 27 hadi 29, 2016.

Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Augustine Mahiga amesema katika ziara ya rais Lungu atatembelea vitengo na sehemu muhimu zinazounganisha nchi ya Tanzania na Zambia kiuchumi.

“Rais Edgar Lungu amealikwa na Dk. Magufuli kutembelea nchini kuanzia Jumapili ya Novemba 27 hadi 29, 2016. Katika ziara yake atatembelea vitengo na sehemu mumihu vinavyounganisha nchi na Zambia kiuchumi ikiwa ni pamoja reli ya Tazara,” amesema.

Ametaja sehemu nyingine atakazotembelea Rais Lungu kuwa ni Bandari ya Dar es Salaam, na kituo cha mizigo kinachohifadhi mizigo inayokwenda Zambia kabla ya kwenda bandarini.

“Siku ya mwisho ya ziara yake, atembelea bandari ya DSM kabla ya kuelekea uwanja wa ndege kwa ajili ya kurudi nchini kwake,” amesema.

Aidha, Mahiga amesema Rais Lungu na Magafuli watasaini baadhi ya mikataba ikiwemo ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara ) ili kulifufua shirika hilo.

Share:

Leave a reply