Kamanda Siro atoa mrejesho wa matukio ya mashambulizi ya Vikindu

567
0
Share:

Jeshi la Polisi kanda maalum ya kipolisi ya Dar es Salaam chini ya Kamanda Simon Siro limetoa mrejesho wa tukio la ujambazi lililotokea  takribani wiki moja na nusu zilizopita katika msitu wa Vikundu.

 Kamanda Siro ametoa mrejesho huo akionyesha baadhi ya silaha na vifaa vilivyotumiwa na  majambazi hao ambao wanahusishwa moja kwa moja na mauaji ya askari Polisi wanne huko nje ya Jiji  la Dar es Salaam eneo la Mbande katika tawi la Benki ya CRDB.

“Katika operesheni tuliyoianza takribani wiki moja na nusu zilizopita tulibaini kuwa kuna mtandao wa majambazi mkubwa unaohusisha raia kutoka Tanzania na Kenya ambao ni majambazi, pia tulifanikiwa kuwatia nguvuni majambazi watatu waliohusika katika tukio la mauaji ya askari wetu eneo la Chang’ombe, na katika mahojiano waliweza kuwataja wenzao na mahali walipo” amesema Kamanda Siro.

“Jeshi la Polisi limezitia nguvuni silaha nyingi sana zilizotumika katika matukio tofauti ya kiuhalifu, ambazo zinatosha kujaa katika amala za silaha, pia tumekamata sare za jeshi la Polisi na mali zilizoibwa katika matukio tofauti ya kiuhalifu” ameongeza Kamanda Siro.

20160905_133123

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Siro akionyesha baadhi ya vitu vilivyokamatwa na Jeshi la Polisi katika mkutano na waandishi wa habari kwenye kituo cha Polisi cha kati leo jijini Dar es Salaam.

 Aidha Kamanda Siro ametoa wito kwa viongozi wa mitaa na vijiji kwa kushirikiana na wananchi wote kwa ujumla wahakikishe kuwa wanatoa taarifa haraka kwa Jeshi la Polisi pale wanapohisi uhalifu ama mtu asiyeeleweka kabla ya madhara kutokea.

 “Labda tu nitoe wito kwa serikali za vijiji na wananchi wote kwa ujumla kwamba jeshi la polisi pekee haliwezi kusaidia kupunguza matukio ya uhalifu, tunahitaji watu wote watoe ushirikiano, unapoona nyumba au chumba hakifunguliwi muda mrefu na wanaoishi hawaeleweki toa taarifa kituoni mara moja” aliongeza Kamanda Siro.

Kwa upande mwingine Bwana Fakhrudeen Tayib Ali mkazi wa Posta jijni Dar es Salaam ametoa kiasi cha Shilingi laki moja kwa msamaria mwema aliyetoa taarifa za majambazi eneo la Vikindu jijini Dar es Salaam, Bw Fakhrudeen ameliomba Jeshi la Polisi kuendelea na kazi nzuri ya kuwalinda raia pamoja na mali zao na kuwaasa wananchi watoe ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.

Silaha

Pichani juu na chini ni baadhi ya vitu mbalimbali vilivyokamatwa kwenye oparesheni hiyo.

“Naomba Jeshi la Polisi liendelee na moyo huo huo wa kuwalinda raia wote na mali zao lakini pia wananchi tusichoke na tusiogope kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili tukomeshe uhalifu” amesema Fakhrudeen.

Baadhi ya  orodha ya silaha zilizokamatwa katika matukio ya uhalifu ya vikindu na mali za wananchi zilizoibiwa katika matukio mbalimbali ya kiuhalifu ni pamoja na Pistol 16 na risasi 558, Radio calls 12, Binoculars 3, Pingu za plastic 45, Bullet proof / body armor 3.

Vingine ni  Mkasi mkubwa wa kukatia vitu vigumu kama minyororo na kufuli, Risasi baridi 37,Tool box, Nyundo, pingu za chuma, Seva/ server ya CCTV  na vingine vingi.

Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC)

20160905_124202

20160905_123852

Bwana Fakhrudeen Tayib Ali mkazi wa Posta jijni Dar es Salaam

Bwana Fakhrudeen Tayib Ali mkazi wa Posta jijni Dar es Salaam.

Magari ya wizi

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Siro akionyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) baadhi ya magari ya wizi yaliyokamatwa kwenye oparesheni hiyo.

Share:

Leave a reply