Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii yapongeza upatikanaji wa dawa za Saratani Ocean road

383
0
Share:

Kamati ya Bunge ya Huduma ya Jamii chini ya Mwenyekiti, Mh Peter Selukamba imetembelea taasisi ya saratani ya Ocean road  na kupata maelezo mbalimbali katika taasisi hiyo.

 Katika ziara hiyo kamati imepongeza na upatikanaji wa dawa za saratani ambao umefanikiwa  kutoka  4%  mpaka 60% katika taasisi hiyo huku kwa upande wa dawa za saratani ya mlango wa kizazi hupatikana kwa asilimia 100 katika taasisi hiyo.

Pia kamati  hiyo imefurahishwa kwa kuona muda wa matibabu kwa mgonjwa kusubiri kutoka miezi mitatu hadi wiki sita ikiwa ni moja ya fanikio kubwa sana kwa taasisi.

Ikiwa ni moja kati ya majumkumu ya kamati hiyo ya HUDUMA ZA JAMII  katika kufuatilia miradi inayotokana  na  jitihada zinazofanywa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kamati hii imeipongeza Wizara ya Afya, ma na kuahidi wataendelea kuisisitiza serikali.

Nae Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameihasa  jamii kuwa na tabia yakupima afya zao mara kwa mara ili kupunguza madhara yatokanayo na magonjwa ya saratani ambayo hushambulia Watanzania wengi kutokana na kuchelewa kupima maradhi hayo.

Kamati hiyo ya Huduma za Jamii ikipatiwa maelezo katika moja ya vitengo vya mionzi kwenye taasisi hiyo ya Ocean road.

Kamati hiyo ikiwasikiliza meza kuu

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akifafanua jambo kwa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii walipotembelea taaisisi ya Ocean road

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii wakifuatilia maelezo kutoka kwa mtaalam wa mionzi (Hayupo pichani)

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa tukio hilo

Share:

Leave a reply