Kamati ya Bunge ya Hudumma za Jamii yatembelea taasisi ya NIMR utafiti dawa asili Dar

441
0
Share:

Kamati ya kudumu ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ile ya Huduma za Jamii mapema leo Machi 24.2017, imetembelea na kukagua mambo mbalimbali  kwenye shughuli zinazofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa ya Binadamu (NIMR)iliyopo Mabibo Jijini Dar es Salaam.

Katika tukio hilo awali Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Utafiti kutoka  Taasisi hiyo ya NIMR, Dk. Julius Massaga alisoma taarifa juu ya shughuli wanazofanya katika kituo hicho cha utafiti wa tiba ikiwemo mradi wa ujenzi wa Maabara na kiwanda cha dawa za tiba asili.

Dk. Massaga aliiambia Kamati hiyo ya Bunge kuwa mradi huo ulianza mwaka 2003 ukiwa na lengo la kuendeleza dawa za asili zilizopo hapa nchini huku ikiwa na lengo la kutafiti dawa za  tiba asili, kuwezesha kuvumbuliwa upya kwa dawa za tiba asili, kuongeza ufanisi wa uhitaji katika kudhibiti tiba  ya magonjwa pamoja na mambo mengine mbalimbali ikiwemo kuchangia pato katika taasisi na Taifa sambamba na  kutoa ajira kwa Umma wa Watanzania.

“Tangua mwaka 2001, NIMR imeendelea  kufanya utafiti wa tiba asili ambapo jumla ya dawa 12 za asili zimevumbuliwa. Dawa hizo ni za kutibu magonjwa mbalimbali pamoja na zile za kuimalisha viungo vya mwili na kinga kwa mambo mbalimbali.” Alieleza Dk. Massaga.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Maendelo ya Jamii Jinsia na Wazee na Watoto, Mh. Himisi Kigwangalla ambaye alikuwa kwa kamati hiyo, amekipongeza kituo hicho kwani kitakuwa kikizalisha dawa zitakazofungashwa kisasa hasa zile za tiba asili.

“Hiki ni kituo cha dawa tiba asili. Lakini pia ni kituo cha kipekee kitakachoaanza kuzalisha dawa zitakazozalishwa kisasa.  Awamu ya kwanza ndio hii tunainza na tunatarajia kuleta mitambo mikubwa nay a kisasa. Utafito wetu unaenda zaidi ya miaka 10 hadi 12.” Ameeleza Dk. Kigwangalla.

Dk. Kigwangalla ameongeza kuwa,  kwa sasa wanamalengo makubwa ya kuanza kuzalisha dawa hizo kwani  miongoni mwa dawa hizo 12, kwa kipindi cha miaka 13 iliyopita na dawa 7 kati ya hizo, zimmeshakamilika kufanyiwa utafit na zitapelekwa kufanyiwa usajili na TFDA na baada ya hapo zitarudishwa hapa ili kufanyiwa package na kuzalishwa kwa wingi  na kwenda kutumiwa na binadamu.

Kuna dawa za nguvu za kiume, kuzuia magonjwa nyemelezi, kuna dawa za Maralia na dawa zingine. Taasisi hii inaendeshwa kitaalam na ni tofauti na utaratibu wa wale wanaosajiliwa na Baraza la tiba asili.” Alimalizia Dk. Kigwnagalla.

Kwa upande wao baadhi ya wabunge ambao ni wajumbe wa  Kamati hiyo waliweza kuhoji mambo mbalimbali ikiwemo suala la mradi wa ujenzi wa jengo hilo pamoja na mitambo inayohitajika kuwa kuna tatizo ambapo ufanisi wa jengo na mitambo hautaakuwa rafiki kwa sasa zaidi wameweza kuchukua maoni yao na mambo mengine kwa ajili ya kufanyia kazi Bungeni. Kamati hiyo iliongozwa na Makamu Mwenyekiti ambaye ni Mbunge wa Ilala, Mussa Hassan Zungu.

Makamu Mwenyekiti ambaye ni Mbunge wa Ilala, Mussa Hassan Zungu akiangalia mtambo mkubwa ambao umefungwwa kwa ajili ya tafiti katika jengo hilo la NIMR Mabibo

Mitambo katika jengo hilo la NIMR Mabibo

Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Utafiti kutoka  Taasisi hiyo ya NIMR, Dk. Julius Massaga akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii ya Bunge walipotembelea taasisi hiyo Dar

Mitambo hiyo ambayo inaendelea kufungwa kama inavyoonekana

Wajumbe wa Kamatiya Huduma za Jamii ya Bunge wakitoka kutembelea jengo hilo

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla (kushoto) akiwa na Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii wakati wa ziara hiyo mapema leo Machi 24.2017, katika ofisi za NIMR Mabibo Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitoa maelezo machache katika tukio hilo

Baadhi ya wajumbe wakifuatilia tukio hilo

Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Utafiti kutoka  Taasisi hiyo ya NIMR, Dk. Julius Massaga akisoma taarifa kwa Kamati hiyo (Haipo pichani)

Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Utafiti kutoka  Taasisi hiyo ya NIMR, Dk. Julius Massaga akitoa ufafanuzi taarifa hiyo

Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi akichangia mawazo wakati wa Kamati yake ya Huduma za Jamii ya Bunge walipotembea NIMR Mabibo

Wajumbe wakitoa maoni yao

Dk. Kigwangalla akitoa maelezo namna ya miradi inayofanywa na NIMR

Baadhi ya dawa ambazo tayari zimefaanyiwa utafiti na kuonekana mara baada ya kuwa katika vifungashio maalum

Baadhi ya dawa hizo kama zinavyoonnekana ambazo zimefanyiwa utafiti wa kina na NIMR ili kwenda kutumika.

Wajumbe hao wakiondoka baada ya kumaliza tukio hilo

Wajumbe wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kwa shughuli za Kamati hiyo ya Huduma za Jamii katika taasisi hiyo ya NIMR ya utafiti wa tiba asili iliyopo Mabibo Jijini Dar es Salaam.

Share:

Leave a reply