Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii yatembelea Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Jijini Dar leo

331
0
Share:

Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii mapema  Machi 29. 2016 imetembelea  Makao makuu ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD)  kwa ajili ya kujionea mambo mbalimbali ya kiutendaji na namna bohari hiyo inavyofanya kazi katika kusambaza dawa zake hapa nchini.

Kamati hiyo inaongozwa na Mh. Peter Serukamba (Mbunge) pamoja na wajumbe mbalimbali wa kamati, wamepata kutembezwa katika maghala ya dawa yaliyo kwenye bohari hiyo na kujionea hali halisi ikiwemo juhudi za Bohari hiyo inavyopata dawa zake kutoka vyanzo tofauti tofauti pamoja na usambazaji wake.

DSC_8242Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii, Mh. Peter Serukamba  (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Mh. Suzan Lyimo (Mbunge wa Chadema). Wengine ni Maofisa wa MSD, Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi wa MSD, Bi. Mary Ringo  pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD, Bw. Fredrick Nicolaus (kulia).

DSC_8217Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi wa MSD, Bi. Mary Ringo akitoa maelezo kwa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii waliotembelea katika Bohari hiyo.

DSC_8234Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii, Mh. Peter Serukamba  (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Mh. Suzan Lyimo (Mbunge wa Chadema). Wengine ni Maofisa wa MSD, Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi wa MSD, Bi. Mary Ringo wakitembelea katika maghala hayo ya MSD.

DSC_8231Kamati hiyo ya kudumu ya Maendeleo ya Jamii ikitoka katika sehemu ya kuhifadhia dawa maalum  ya hali ya ubaridi.

DSC_8227eneo la maghala ya MSD upande wa dawa maalum za miradi Msonge kama zinavyoonekana

DSC_8235Wabunge wakitoka katika ghala maalum la kuhifadhia dawa maalum za Msonge…

DSC_8275Mh. Jacqueline Ngonyani (Mbunge)  akitoka kuangalia moja ya mafriza yanayohifadhia dawa maalum za matumizi ya kila siku wakati wa Wajumbe wa Kamati ya  Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii.DSC_8281 Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi wa MSD, Bi. Mary Ringo akiwaonesha Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii ya Bunge namna madawa yaliyokwisha muda wake yanapohifadhiwa.

DSC_8303

Baadhi ya madawa ambayo yamekwisha muda wake kama yanavyoonekana ndani ya maghala ya MSD

DSC_8294Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa ufafanui wa namna ya madawa hayo yanavyohifadhiwa katika maghala hayo. kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Mh. Jacqueline Ngonyani  na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ha Maendeleo ya Jamii, Mh. Surukamba. DSC_8259Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwaonyeshea wabunge namna dawa hizo zinavyohifadhiwa katika mafriji maalum

DSC_8297Mbunge wa Viti Maalum, Mh. Jacqueline Ngonyani akiuliza swali namna dawa ambazo hazipewi kipaumbele kufikishwa katika vituo vya Afya.

DSC_8276Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii, Mh. Peter Serukamba (kushoto) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mh. Hazzan Zungu.

DSC_8240Kamati hiyo ikielekea katika maghala ya kuhifadhia dawa ndani ya MSD.DSC_8246Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bwana Laurean Bwanakunu (katikati) akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla walipotembelea katika maghala hayo.

DSC_8242Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD, Bw. Fredrick Nicolaus akiwaongoza Kamati ya Maendeleo yaa Jamii kwenye maghala ya MSD wakati walipotembelea bohari hiyo.

DSC_8248Baadhi ya maafisa wa Wizara ya Afya na Bunge wakiwa kwenye msafara huo wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii walipotembelea MSD.

DSC_8310DSC_8202Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo namna ya maghala hayo yanavyohifadhi dawa na namna ya kusambaza katika Hospitali za hapa nchini. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

Share:

Leave a reply