Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii yatembelea mfuko wa BIMA ya Afya (NHIF) yapongeza

556
0
Share:

Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii mapema jana Machi 17.2016 imetembelea  Makao makuu ya Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) jijini Dar es salaam na kuweza kupewa  taarifa mbalimbali za kiutendaji pamoja na mipango yao ya baadae na changamoto mbalimbali zinazoikabili taasisi hiyo.

Aidha, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo waliweza kujibu mambo mbalimbali yaliyoulizwa kwao kama viongozi wenye dhamana na mfuko huo wa Bima ambapo Kamati hiyo iliyo chini ya Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati walipongeza  juhudi za mfuko huo huku wakitaka kufanyia marekebisho kadhaa yanayojitokeza mara kwa mara.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael Mhando ameiambia kamati hiyo kuwa, mipango mbalimbali inaendelea kuona namna ya kufanyia maboresho ambapo baadhi ya changamoto zingine wanazokabiriana nazo zinatokana na mifumo  wa kisera hivyo endapo watatakiwa kuzibadilisha basi watafanya hivyo kwa mujibu wa sharia.

Kwa upande wa Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, miongoni mwa ongezeko la mapato na maendeleo katika sekta ya Afya hapa nchini, mfuko huo umekuwa ni chachu kubwa akitolea Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Aidha, Kamati hiyo pia imepata kuoneshwa na kupata maelezo ya namna ya mfumo wa ufanyaji kazi kwa njia ya Teknohama ambapo waliwahakikishia wabunge hao kuwa, mfumo huo upo salama na unatoa huduma kwa njia bora na ya kisasa hivyo taarifa zote zinahifadhiwa na kufanyiwa kazi za wanachama wote.

DSC_7404Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Maendeleo ya Jamii, Dkt Raphael Chegeni akiongoza kamati hiyo walipotembelea Makao makuu ya NHIF jijini Dar es Salaam

DSC_7396Baadhi ya Wabunge walio kwenye kamati hiyo ya Maendeleo ya Jamii wakifuatilia mkutano huo

DSC_7399Baadhi ya Wabunge walio kwenye kamati hiyo ya Maendeleo ya Jamii wakifuatilia mkutano huo

DSC_7382 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa taarifa ya Wizara yake kwa Kamati hiyo ya Maendeleo ya Jamii.

DSC_7383Wakifuatilia mkutano huo

DSC_7386Baadhi ya wafanyakazi wa NHIF wakifuatilia mkutano huo

DSC_7466Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akitoa taarifa katika kamati hiyo..

DSC_7473 Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael Mhando akitoa taarifa ya utendaji wa mfuo huo ..

DSC_7477Mkurugenzi wa Teknohama wa NHIF, Makao Makuu, Bw.Ali Othman akitoa maelezo ya kitaalam juu ya mifumo ya tehama inavyofanya kazi na namna wanavyoboresha huduma zao hizo

DSC_7490Mkurugenzi wa Usimamizi Tiba wa NHIF, Dk. Frank Lekey akitoa maelezo yake kwa kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii walipotembelea Makao Makuu ya ofisi hizo

DSC_7485Mkurugenzi wa Teknohama wa NHIF, Makao Makuu, Bw.Ali Othman akitoa maelezo ya namna ya tehama inavyofanya kazi hasa katika kuboresha huduma kwa wateja wao.

DSC_7388Baadhi ya watendaji waandamizi wa NHIF wakifuatilia kupitia simu zao namna ya mfumo huo wa tehama unavyofanya kazi  kwa mteja kupitia simu za mkononi kuwa na uwezo wa kuhakiki. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

Share:

Leave a reply