Kamati ya Nidhamu ya TFF yamfungia Juma Nyoso mechi tano

143
0
Share:

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) imemfungia Mchezaji wa Timu ya Kagera Sugar, Juma Nyoso kutocheza mechi tano baada ya kumtia hatiani kwa kutaka kumpiga shabiki, kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ambapo timu yake ilicheza na Simba.

Katika hatua nyingine, Kamati ya Nidhamu ya TFF imempiga faini ya Shilingi milioni moja Juma Nyoso.

Vilevile, Kamati hiyo imemfungia Mchezaji wa Transit Camp, Mohamed Ussi kutocheza mechi tatu kutokana na utovu wa nidhamu kwa kutaka kumpiga  mwamuzi wa mchezo.

 

Ussi alifanya kosa hilo katika mechi namba 48 ya kundi C Ligi Draja la Kwanza Tanzania Bara.Kamati ya Nidhamu pia imempiga faini ya shilingi laki tatu Ussi.

Share:

Leave a reply