Kampeni ya Declutter&Donate yaanza kufanyika Dar, lengo la kusaidia wanawake na watoto

261
0
Share:

Kwa kutambua changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili wanawake wanaoishi katika mazingira magumu kampuni ya Elite Organizing Services Limited Septemba, 13 ya mwaka huu ilifanya uzinduzi wa Kampeni ya Declutter&Donate ambayo ina lengo la kusaidia wanawake na watoto, sasa kampeni hiyo imeanza kufanyika jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia siku ya kwanza ya kampeni hiyo ambayo inaendeshwa kwa kukusanya vitu mbalimbali vya nyumbani na maofisini ambavyo vinakuwa havitumiki, Mkurugenzi wa Kampuni ya Elite Organizing Services Limited na mwanzilishi wa kampeni ya Declutter&Donate, Nasra Karl Mbululo alisema mapokeo ya kampeni hiyo hayajawa makubwa lakini kwa wachache ambao wamejitokeza wameweza kuchangia vitu ambavyo wanakusudia kuvikusanya.

fb909370-fd1e-4c5b-91cd-fb85e7dac5a9Mkurugenzi wa Kampuni ya Elite Organizing Services Limited na mwanzilishi wa kampeni ya ya Declutter&Donate, Nasra Karl Mbululo akipokea vifaa vya kuchezea watoto kutoka kwa Safwaan Khatri.

“Tunachukua vifaa vya michezo, midoli, vitabu, samani za nyumbani na ofisini, tv, redio deki na vitu vingine visivyotumika na mwamko umekuwa mdogo lakini kwa waliojitokeza wametoa vitu vizuri ambavyo tumekuwa tukivitaka, siku ya kwanza imekuwa na watu wachache lakini imekuwa siku nzuri kwa kukusanya tunachohitaji,

“Kampeni hii imeanzishwa ikiwa na malengo ya kusaidia wanawake ambao wanaishi katika mazingira magumu na watoto, na leo ni siku ya kwanza lakini tunataraji kwenda kufanya na sehemu nyingi ili kukusanya na baadae tukawasaidie watu ambao tumewakusudia,” alisema Nasra.

ced4e135-01fd-4cfd-94d1-627020fd02ffMkurugenzi wa Kampuni ya Elite Organizing Services Limited na mwanzilishi wa kampeni ya ya Declutter&Donate, Nasra Karl Mbululo akimwelekeza jambo, Taiba Khatri kuhusu Kampeni ya Declutter&Donate.

Alisema baada ya zoezi hilo kuendeshwa katika Shule ya Sekondari Tambaza, wanataraji kulifanya tena Oktoba, 16 katika Shule ya Msingi Oysterbay, na baada ya hapo watatangaza sehemu nyingine ambazo zitafuatia.

Alisema kuwa baada ya zoezi la ukusanyaji kumalizika watakwenda kutoa semina inayohusu afya kwa wanawake wanaoishi Mabwepande na kisha kwenda katika kituo cha kulelea watoto kwa ajili ya kuwapatia msaada ambao umepatikana kutokana na zoezi ambalo wanalifanya sasa la kukusanya vitu ambavyo havitumiwi majumbani na maofisini.

bd6e6286-cfee-4adc-8f57-f3f98f7268dbMkurugenzi wa Kampuni ya Elite Organizing Services Limited na mwanzilishi wa kampeni ya Declutter&Donate, Nasra Karl Mbululo na Esther Daffa wakipanga vitu ambavyo vimetolewa na watu ambao wametembelea kituo cha Shule ya Sekondari Tambaza.

“Disemba, 15 tutatoa semina ya afya ya mwanamke na hedhi salama na watapata nafasi ya kufanyiwa uchunguzi na kuzungumza na madaktari kisha tutawapatia taulo za hedhi (pad), tumekadiria ziwe za miezi sita,

“Baada ya hapo, Disemba, 20 tutakwenda kutoa msaada kwa kituo cha watoto ambacho tutakitaja hapo baadae kwahiyo niwaombe watu ambao wana vitu ambavyo sisi tunavihitaji watupatie ili vitumike kuwasaidia wengine,” alisema Nasra.

Share:

Leave a reply