Kampuni ya Amazon kuajiri wafanyakazi 100,000

1335
0
Share:

Kampuni ya kuuza bidhaa kwa njia ya mtandao ya Amazon yenye makao makuu yake Marekani imetangaza nia yake ya kuajiri wafanyakazi 100,000 ndani ya kipindi cha miezi 18 ijayo.

Katika taarifa ambayo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Amazon, Jeff Bezos imesema kuwa Amazon imepanga kutoa ajira 100,000 za moja kwa moja ili mpaka mwaka 2018 wawe na wafanyakazi 280,000 kutoka 180,000 ambao wanao sasa.

“Ajira zote sio kwa ajili tu ya makao yetu makuu Seattle au Silicon Valley, watakuwa wakitoa huduma kwa wateja wetu na shughuli zingine kwa watu wetu waliopo sehemu zingine,” amesema Bezos.

Mpaka Disemba 31, 2015 kampuni ya Amazon ilikuwa na wafanyakazi 230,800 ambao walikuwa wana ajira ya moja kwa moja na wengine wakiwa wanalipwa kwa muda ambao wanakuwa kazini.

Share:

Leave a reply