Kampuni ya Elite Organizing Services yatoa msaada wa pad kwa wanawake wa Mabwepande

429
0
Share:

Zikiwa zimepita siku 96 tangu kuzindua kampeni ya Declutter&Donate ambayo ina lengo la kuwasaidia watoto wenye mahitaji na wanawake ambao wanaishi Mabwepande, Dar, hatimaye kampuni ya Elite Organizing Services Limited imekamilisha ahadi ya kuwapa msaada wa taulo za hedhi wanawake wa Mabwepande pamoja na kuwapa elimu kuhusu hedhi salama.

Akizungumza kuhusu msaada huo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Elite Organizing Services Limited na mwanzilishi wa kampeni ya Declutter&Donate, Nasra Karl Mbululo alisema wameona ni vyema kuanza na wanawake wa Mabwepande kutokana na changamoto ambazo zinawakabili kwani lengo lao ni kuwasaidia wanawake ambao wanaishi katika mazingira magumu.

dsc_1898Mkurugenzi wa Kampuni ya Elite Organizing Services Limited na mwanzilishi wa kampeni ya Declutter&Donate, Nasra Karl Mbululo akizungumza na wanawake ambao wanaishi Mabwepande wakati wakipewa elimu kuhusu hedhi salama.

“Kampeni ya Declutter&Donate ndiyo imefanyika kwa mara ya kwanza na sehemu ya kwanza tulichagua Mabwepande, tumechagua hapa sababu wakazi wa hapa waliathirika na mafuriko ya mwaka 2012, huu ni mji mpya na una changamoto zake, serikali inafanya kwa nafasi yake na wananchi kwa sehemu yake, sisi tunafanya kazi sehemu ya wananchi kupunguza changamoto za wakazi wa Mabwepande,

“Lengo letu ni kufika sehemu zote ambazo zina mazingira magumu kwa mwanawake lakini inabidi kuanza taratibu ili kuona kile unachokifikiria ni kweli kinaleta mabadiliko kwa jamii, na tumeona tuanze Mabwepande tulete semina na tuone manufaa yake na vile vitu ambavyo havikuleta mabadiliko chanya turekebishe ili tusogee kwenda sehemu nyingine na lengo kufika sehemu yoyote Tanzania,” alisema.

dsc_1906

Aidha Nasra alizungumza kuhusu sehemu ya kwanza ya kampeni hiyo ya Declutter&Donate kuwa mwamko wa watu kutoa vitu ambavyo hawavitumii haukuwa na jinsi walivyotegemea lakini wamejifunza kipi kinatakiwa kufanyika.

Pia Nasra alitoa wito kwa jamii na Watanzania na kusema “Jamii kumsaidia mwenzako sio lazima umpe pesa, tuangalie jambo gani unaweza kumsaidia mwenzako, wananchi wajifunze jambo jipya kuwasaidia watu wenye uhitaji maalumu.”

dsc_1961Mfaidika wa msaada wa Declutter&Donate, Rhoda Mwinami akielezea jinsi ambavyo wameelimika kutokana na elimu ya hedhi salama waliyopewa pamoja na kupewa taulo za hedhi ‘pad’ za kutumia.

Nae mmoja wa wafaidika na msaada Rhoda Mwinami alisema elimu ambayo wamepatiwa imewasaidia kufahamu mambo ambayo hawakuwa wakifahamu awali kuhusu hedhi na hivyo itawasaidia kujitunza na kuwa wasafi hali ambayo itawapunguzia hata baadhi ya magonjwa yanayotokana na usafi katika kipindi cha hedhi.

“Tumejifunza jinsi ya kujitunza na hedhi salama … kabla ya kupata elimu tulikuwa tunajua tukiingia unatumia kitambaa au kutumia pad lakini jinsi ya kufanya usafi mara ngapi tulikuwa hatujui lakini sasa hivi tumejua jinsi ya kufanya, nimepanga takuwa nakutana na mabinti na kuwaeleza jinsi gani wanatakiwa kujitunza,” alisema Rhoda.

dsc_1957Mwenyekiti wa mtaa wa Mji Mpya uliopo kata ya Mabwepande, Justin Chiganga akizungumza na wananchi wake kuhusu ahadi ya kampuni ya Elite Organizing Services Limited ya kuwapelekea elimu ya hedhi salama na msaada wa pad wakazi wa eneo hilo.

dsc_1958

dsc_1981Mkurugenzi wa Kampuni ya Elite Organizing Services Limited na mwanzilishi wa kampeni ya Declutter&Donate, Nasra Karl Mbululo akiongoza timu ya Declutter&Donate kugawa taulo za hedhi ‘pad’.

dsc_1989

dsc_2023Timu ya Declutter&Donate ikiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanufaika wa elimu ya hedhi salama na msaada wa taulo za hedhi ‘pad’.

Share:

Leave a reply