Kampuni ya JAVIS International trade Co.ltd watoa huduma ndani ya Sabasaba

517
0
Share:

Kampuni ya JAVIS  International trade Co.ltd ambao wapo kwenye banda la Jakaya Kikwete kwenye mabanda ya Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam wanawatangazaia wananchi mbalimbali kujitokeza kwa wingi kuchangamkia huduma zao mbalimbali zinazotolewana kampuni hiyo ambazo ni rahisi na zina unafuu kwa kila Mtanzania ama mtu yoyote ambaye atapata huduma kutoka kwao.

JAVIS inajihusisha na uagizaji, uuzaji na usafirishaji wa bidhaa nje na ndani  ya nchi. Ambapo wamejikita zaidi katika biashara ya Kimataifa na biashara ya kieletroniki.

“Tupo hapa kuboresha biashara yako, utendaji na kukupa ufumbuzi wa mafanikio ya biashara. Tunaunda jamii ya kisasa ya biashara  kwa wateja wetu ili waweze kufanya biashara  kwa urahisi popote walipo na kwa ufanisi.” Walieleza JAVIS.

JAVIS inawakaribisha wateja wote wanaohitaji kuagiza vitu nje ya nchi kujitokeza kwa wingi kupata maelezo zaidi na aina ya huduma zao wanazotoa kwani zipo kwa njia bora na za kisasa huku wakisamini mchango wa mteja kwa kumpa huduma bora, bei nafuu huku wakiw ana njia mbalimbali za malipo ya ununuzi kwa wateja wote waaminifu.

Mbali na Sabasaba, JAVIS wanapatikana Jijini Dar es  Salaam, katika jingo la Ushirika gorofa ya 4, Mtaa wa Kariakoo, Lumumba. Ama unaweza kuwasiliana nao kupitia: www.ejavis.com

Alic Mathias  kutoka JAVIS akiwa tayari kukuhudumia katika banda lao hilo ndani ya Sabasaba

Baadhi ya wananchi wakipata kusoma mabango ndani ya banda hilo

Baadhi ya huduma zao wanazotoa JAVIS

Banda hilo ndani ya Sabasaba

Omary Kizango wa JAVIS akizungumza na wateja waliofika kupata huduma katika banda hilo

Share:

Leave a reply