McDonald’s yamwomba msamaha Rais Trump kwa kumwandika vibaya

362
0
Share:

Kampuni ya McDonald’s ambayo ndiyo wamiliki wa migahawa ya McDonald’s iliyosambaa maeneo mbalimbali duniani imeomba msamaha kwa Rais wa Marekani, Donald Trump baada ya akaunti yake ya Twitter kuweka maeneno ambayo yalikuwa yakimsema vibaya Trump.

Katika taarifa ambayo imetolewa na kampuni hiyo ilieleza kuwa si wao ambao walifanya kitendo hicho bali ni wahalifu wa mtandaoni (hackers) ambao walikuwa wameiba akaunti hiyo na kuweka ujumbe huo ambao ni wazi haukuwa na maneno mazuri ya kufurahisha.

“Kwa uchunguzi ambao tumeufanya tumebaini kuwa akaunti yetu ya Twitter ilikuwa imeibiwa. Tulichukua hatua ili kuilinda, na tunaomba radhi kwa ujumbe ambao ulikuwa umewekwa kwenye akaunti yetu,” alisema msemaji wa McDonald’s, Terri Hickey katika taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo.

Ujumbe ambao ulikuwa umewekwa kwenye akaunti ya McDonald’s ulikuwa ukisema,”@realdonaldtrump kwa kweli Urais wako unatatiza sana, tunapenda arudi @BarackObama”

Share:

Leave a reply