Kampuni ya simu ya Verizon yainunua Yahoo kwa Dola Bilioni 4.8

233
0
Share:

Katika kuhakikisha inazidi kuwa kampuni kubwa ya mawasiliano duniani na kuwafikia watu wengi zaidi, kampuni ya simu ya Marekani, Verizon imetangaza kuiunua kampuni ya mawasiliano na teknolojia ya Yahoo kwa kiasi cha pesa cha Dola Bilioni 4.8.

Katika taarifa ambayo imethibitishwa na Verizon kupitia mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, Lowell McAdam na kueleza kuwa wamefanikiwa kuipata Yahoo na sasa wanaamini kampuni yao itazidi kuwa moja ya makampuni bora duniani.

Alisema kuwa kabla ya kutaka kuinunua Yahoo walitaka kununua kampuni ya mawasiliano yya habari ya AOL lakini ilishindikana na ndipo Mei, 2015 wakaanza harakati za kuinunua Yahoo ambayo awali ilikataa kiasi cha pesa ilichopeleka kwa ajili ya kuinunua.

“Kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita tuliomba kuipata AOL ili kutimiza mipango yetu ya kuboresha huduma zetu za mawasiliano kwa wateja wetu na kampuni ambazo tunatangaza,

“Kuipata Yahoo kutaiweka Verizon katika ushindani wa juu na kuwa kampuni kubwa ya mawasiliano ya simu duniani na kutusaidia kukuza mapato yetu kwa kuboresha matangazo yetu,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Verizon.

Biashara ya Verizon kuinunua Yahoo itaiwezesha kampuni ya Verizon kuwa mmiliki halali wa mtandao wa Yahoo pamoja na program tumishi za Yahoo.

Share:

Leave a reply