Kanisa la Pool of Sloam latoa msaada wa matairi kituo cha Polisi Nguruka, Kigoma

372
0
Share:

Kupitia jitihada za zinazofanywa na Asasi, taasisi,makampuni na watu binafsi,kwa kuunga mkono juhudi za Serikali kwa lengo la kukamilisha huduma mbalimbali kwa Umma, Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma amepokea jumla ya  matairi matairi yenye thamani ya shilingi millioni mbili na laki nane ili  kuboresha gari la polisi la kituo cha Nguruka kata ya Nguruka wilayani Uvinza.

Akipokea mataili hayo yaliyotolewa na kanisa la Pool of  Sloam,kwa niaba ya Naibu kamishina wa polisi Mkoani Kigoma,Ferdinand  Mtui,mkuu wa polisi wilaya ya Uvinza Amedeus Malenge amesema kuwa kitendo kilichofanywa na kanisa hilo kitasaidia kuifikia jamii kwa  wakati hasa wahalifu.

Kwa upande wake Kuhani Ufahamu Hakikazi  ambaye alimwakilisha kiongozi mkuu wa kanisa hilo hapa nchini,amesema  kuwa baada ya kupata taarifa ya uhitaji wa mataili hayo,kanisa limechukua hatua hiyo kwa kuwa kanisa na Serikali hufanya kazi pamoja  katika kukamilisha huduma za kijamii.

Aidha kuhani Hakikazi ameongeza kuwa ,kupitia mahitaji ya kuboreshwa kituo cha polisi  kilichopo kijijini humo,amesema kuwa amelichukua na atalifikisha kwa  uongozi wa kanisa ili kuona namna linavyoweza kufanyiwa ufumbuzi wa  kuboresha kituo hicho.

Nao viongozi wa kijijini humo akiwemo  mwenyekiti wa kijiji cha nguruka Bw.Mosha Mohamed na mwenyekiti wa  kitongoji cha nguruka kusini Hamis Kiliza,wamesema kuwa kwa kuwa huduma

ya polisi inauhitaji mkubwa kwa jamii,mataili hayo yatasaidia kupunguza  uhalifu kwa kuwa kazi sasa zitafanyika kwa wakati huku wakiomba  kuboreshwa tena kwa kituo hicho cha polisi kwa kuwa sasa hakitoshi kutoa huduma kulingana na wingi wa wahalifu wanaowekwa ndani ya kituo hicho.

Na Abel Daud,KIGOMA

Matairi hayo yaliyokabidhiwa katika kituo hicho cha polisi Nguruka.

 Kuhani Ufahamu akipeana mkona na Mkuu wa Polisi wilaya ya Uvinza mara baada ya kumkabidhi mataili hayo.

Zaoezi hilo la kutoa msaada wa mataili likiendelea katika kituo hicho cha Polisi Nguruka.

Share:

Leave a reply