KCB yatoa milioni 325 kudhamini Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2017/2018

305
0
Share:

Benki ya KCB imeingia mkataba wa mwaka mmoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) wenye thamani ya milioni 325 kudhamini Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa msimu wa 2017/2018.

Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo, Rais wa TFF, Wallace Karia ameishukuru benki ya KCB na kusema kuwa udhamini huo ni muhimu kwani utasaidia kuboresha Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambayo kwasasa msimu wa 2017/2018 unaendelea.

“TFF na benki ya KCB ni taasisi zenye mafanikio benki imedumu kwa zaidi ya miaka 100 vivo hivyo mpira wa miguu nchini … makubaliano haya ni ushahidi kuwa benki kubwa kama KCB inaamini katika mpira kupitia uongozi wa TFF,” amesema Kiria.

Nae wa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania, Cosmas Kimario alisema wanafuraha kuwa sehemu ya wadhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwani kupitia udhamini huo vijana wengi watafaidika na utasaidia kuleta maendeleo ya soka nchini.

“Tunapenda kuiunga mkono TFF katika lengo la kupeleka soka la Tanzania mbele, tunayofuraha kubwa kudhamini ligi Kuu Soka Tanzania Bara, tunaamini michezo inaleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii ni pia chanzo cha ajira kwa vijana na burudani pia,” alisema Kimario.

 

Share:

Leave a reply