Kichuya aimaliza Azam, Simba yapaa kileleni katika msimamo wa VPL

294
0
Share:

Ligi Kuu ya Vodacom Jumamisi ya Septemba, 17 imeendelea kwa michezo mitano kupigwa katika viwanja mbalimbali, mchezo mkubwa ukiwa wa Azam iliyokuwa mwenyeji wa Simba katika uwanja wa Uhuru.

Mchezo huo umemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila, goli la Simba likifungwa na Shiza Kichuya katika dakika ya 65, goli lililodumu hadi dakika ya mwisho ya mchezo huo.

Kwa ushindi huo sasa Simba imepaa hadi kileleni kwa VPL ikiwa na alama 13, ikifuatiwa na Yanga iliyo na alama 10, sawa na Azam zikiwa na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Matokeo ya michezo mingine ni;
Mwadui 0 – 2 Yanga
Mbeya City 0 – 0 Prisons
Mtibwa Sugar 2 – 0 Kagera Sugar
Ruvu Shooting 0 – 1 Mbao FC

Share:

Leave a reply