Kichuya avuruga sherehe ya Yanga, Simba yaendeleza rekodi ya VPL 2016/2017

437
0
Share:

Mchezo wa VPL kati ya mahasimu wa jadi, Yanga na Simba umemalizika kwa timu hizo kumaliza dakika 90 kwa kufungana goli moja kwa moja, Yanga ikiwa ya kwanza kupata goli katika dakika ya 26 kupitia kwa Amissi Tambwe na Simba ikisawazisha goli hilo katika dakika ya 87 kupitia kwa Shiza Kichuya.

Aidha mchezo huo umeshuhudiwa mashabiki wa Simba wakivunja viti vya Uwanja wa Taifa kwa kumlaumu mwamuzi Juma Mgunda kuwa goli lililofungwa na Tambwe halikuwa sahihi kwani Tambwe alishika mpira kwa mkono kabla ya kufunga na pia tukio hilo lilipelekea nahodha wa Simba, Jonas Mkude kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumpiga ngumi mwamuzi.

Pia Simba imeendeleza rekodi ya msimu wa 2016/2017 kwa kutokufungwa mchezo hata mmoja kati ya michezo saba iliyocheza mpaka sasa, ikishinda mitano na kutoa sare mwili, kama utakuwa na kumbukumbu nzuri, msimu ulipita Simba ilipoteza mchezo wa saba ilipokutana na Yanga na kufungwa goli 2-0.

Kwa matokeo ya mchezo wa Yanga na Simba, Simba sasa imefikisha alama 17 ikiwa kileleni kwa msimu wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Yanga ikifikisha alama 11 ikiwa katika nafasi ya tatu ya msimamo wa VPL.

Share:

Leave a reply