Kifo cha Reeva Steenkamp champeleka Oscar Pistorius gerezani miaka sita

233
0
Share:

Mahakama nchini Afrika Kusini imemhukumu mwanariadha wa nchi hiyo, Oscar Pistorius kifungo cha miaka sita kwa kosa la kumuua kwa kudhamiria aliyekuwa mpenzi wake, Reeva Steenkamp mwaka 2013.

Hatia ya Pistorius kukutwa na kosa hilo ilitolewa mwaka jana mwezi Disemba baada ya majaji kukutana na kujadili kifo cha Reeva kilivyotokea na kutoa uamuzi wa kuwa kifo hicho nicha kudhamiria na hivyo kesi yake kubadilishwa kutoka kosa la kuua bila kudhamiria hadi kuua kwa kudhamiria na hivyo kesi kutakiwa kutolewa hukumu upya.

Baada ya huku kutolewa Pistorius amepelekwa moja kwa moja gerezani na upande wa mshitaki na utetezi wanaruhusiwa kukata rufaa ya kesi hiyo lakini mawakili wa Pistorius wamesema kuwa wao hawataka rufaaa hivyo ni wazi mteja wao atakwenda kutumikia kifungo cha miaka sita gerezani labda tu kama atatumia mawakili wengine.

Ikumbukwe Pistorius alimpiga risasi nne aliyekuwa mpenzi wake, Reeva Steenkamp, Februari 2013 kwa madai kuwa akijua ni muharifu.

Share:

Leave a reply