Kigamboni Marathon kufanyika Desemba 2, Kigamboni Dar

588
0
Share:

Katika jitihada za kuijengea Jamii uelewa na hamasa juu ya umuhimu wa kutunza afya na Kufanya Mazoezi, Kampuni ya E World (Events World) kwa kushirikiana na wadau mbali mbali inawaletea mbio za Kigamboni Marathon, mbio hizi zitaambatana na zoezi la Upimaji wa afya katika kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani ambayo huazimishwa tarehe 1 mwezi wa 12 kila mwaka.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Ndg. Dimo Debwe Mitiki Mkurugenzi wa Events World alisema, Lengo kuu la “Kigamboni Marathon” ni kutangaza fursa za uwekezaji, vivutio vya kitalii na Biashara zilizopo Kigamboni kwa maendeleo ya Taifa letu.

Aidha “Kigamboni Marathon” inafanyika kuunga mkono kampeni ya Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha Watanzania kufanya mazoezi ili kuimarisha afya.

Pia Kwa siku za hivi karibuni Tumeshuhudia Viongozi wetu wakihamasisha wafanyabiashara na wadau mbali kuwekeza ndani ya wilaya yetu mpya ya kigamboni, hivyo ni imani yetu kuwa kufanyika kwa ‘kigamboni Marathon’ kutawavutia watu mbali mbali kufika Kigamboni na kujionea uzuri pamoja na fursa zilizopo kigamboni.

Nae Mratibu wa Mbio hizo Mr. Juma K. Mtetwa alisema ni ukweli ulio wazi ya kuwa Kigamboni imezunguukwa na maeneo mazuri zaidi ya kimichezo, Utalii na Uwekezaji kuliko sehemu yeyote ile Jijini Dar es saalam na hiyo ni sababu moja wapo inayotupelekea kuamini kuwa ‘Kigamboni Marathon’ itakuwa ni miongoni mwa mbio bora zaidi Tanzania itakayoibua wakimbiaji wazuri watakao watakaoleta ushindani mkubwa katika Mchezo huu wa riadha Duniani kote.

Kigamboni Marathon imepangwa kufanyika katika viwanja vya mji mwema jirani na ofisi za Halmashauri mpya ya kigamboni tarehe 2 mwezi wa 12, 2017 ikiwa na Mbio za urefu wa kilomita 21(Half Marathon), Kilomita 10 na Mbio kwaajili ya watoto, wazee na hata wale wasio na mazoezi ya mara kwa mara (Fun Run) pia zawadi mbali mbali kushindaniwa zikiwemo Medali za dhahabu, Silver na Gold pia Pesa Taslimu kwa washindi.

Kwa niaba ya Kamati ya maandalizi ya ‘kigamboni Marathon’ natanguliza Shukrani kwa wadau wote waliojitokeza kuunga mkono katika Jambo hili lenye tija kwa Maendeleo ya Taifa letu wakiwemo Viongozi wetu ndani na nje ya Kigamboni, wanahabari, Taasisi Mbali mbali, Makampuni na Jamii kwa Ujumla.

Pia alizishukuru kampuni zilizojitokeza kudhamini mbio hizo ikiwemo Property International, Itel Mobile, Coca cola kupitia kinywaji cha Dasani, J.P.M Hospital, Akemi Restaurant, PCMC Hospital na Red Bull na kuomba wadau na makampumi mbali mbali kujitokeza na ku- support mbio hizo.

Alisema Ushiriki wa Makampuni makubwa kutoka ndani na Nje ya Kigamboni unatoa fursa kwa wafanyabiashara waliyopo Kigamboni na kuwasihi wanakigamboni kuitumia fursa hiyo kujumuika pamoja na kuonyesha walichonacho lakini pia kufahamiana na kuongeza Marafiki wenye tija.

Napenda kuchukua fursa hii pia kuwakaribisha Wadhamini,Washiriki na Wadau mbalimbali katika tukio hili la Kipekee lenye Usalama na Ustaarabu wa Hali ya juu.

Kwa maelezo juu ya ushiriki tafadhari wasiliana na: 0784 959 509 / 0753 777 666, email:[email protected]

Njooni tuungane kwa Pamoja na Kuyapa Thamani Maisha yetu,

“EXPLORE, HAVE FUN AND RUN FOR HEALTHY”.

 Mkurugenzi wa Events World Dimo Debwe Mitiki akizungumza na waandishi wa Habari juu ya lengo kuu la “Kigamboni Marathon” wakati wa utambulisho rasmi kwa wanahabari. Ambapo alieleza kuwa ni pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji, vivutio vya kitalii na Biashara zilizopo Kigamboni kwa maendeleo ya Taifa letu.

 Mkurugenzi wa Events World Dimo Debwe Mitiki akizungumza na waandishi wa Habari juu ya lengo kuu la “Kigamboni Marathon” wakati wa utambulisho rasmi kwa wanahabari. Ambapo alieleza kuwa ni pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji, vivutio vya kitalii na Biashara zilizopo Kigamboni kwa maendeleo ya Taifa letu.

Share:

Leave a reply