Kigwangalla atoa siku 30 kwa wavamizi wa Ngitili kuondoka

210
0
Share:

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa siku 30 kwa watu wote waliovamia hifadhi ya misitu maarufu kama “Ngitili” kuondoa haraka.

Hatua hiyo inalenga kukabiliana na uharibifu wa mazingira uliosababishwa na watu kuvamia mistu hiyo chini ya Mradi wa Hifadhi Aridhi Shinyanga(HASHI).

Waziri huyo alitoa kauli hiyo hivi karibuni Wilayani Kishapu wakati wa kilele cha wiki ya upandaji miti nchini ambapo Kitaifa ilifanyika Mkoani Shinyanga.

Alisema Ngitili zilianizshwa kwa lengo la kuresha uoto wa asili mkoani humo lakini baadhi ya watu wachache wasiitakia mema Shinyanga wameingia katika maeneo hayo na kujimilikisha huku kuendesha shughuli ambazo ni kinyume cha uhifadhi wake.

Dkt. Kigwangala alisema baada ya siku hizo kumalizika kama wahusika hawatakuwa wameondoka wenyewe kwa hiari itabidi nguvu itumike kuwaondoa ili kunusuru uharibifu usiendelee Zaidi katika maeneo hayo kwa ajili ya ustawi wa eneo hilo na nchi kwa ujumla.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema wataendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya uvamizi wa hifadhi za mistu na baada ya elimu hiyo itawabidi watumie nguvu kwa watu wote ambao hawatakuwa tayari kubadilika.

Alisema sanjari na elimu hiyo alitoa wito wa kuimarisha nguvu katika matumizi majiko yanayotumia nishati kidogo nay ale ya gesi ili kunusu mistu nchini.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack aliwataka watendaji wote kuanza kuwaondoa wavamizi wa vyanzo vya maji na mistu.

Aidha aliomba juhudi za usamabazaji wa gesi kwa ajili ya kupikia vijiji uongezwe ili kuwasaidia wananchi kuachana na matumizi ya mkaa na kuni ambazo zinachangia kumaliza mistu.

Naye Meneja wa Wakala wa Mistu Tanzania(TFS) Kanda ya Magharibi Valentine Msusa alisema wanayo orodha ya Ngitili zote zilikuwa zimehifadhi chini ya mradi HASHI na wanatarajia kukikabidhi kwa uongozi wa Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya hatua zaidi.

Maadhimisho ya mwaka huu yalikuwa na kauli mbiu isemayo Tanzania ya Kijani Inawezekana , Panda Miti kwa Maendeleo ya Viwanda.

Na Tiganya Vincent

Share:

Leave a reply