Kim Kardashian aibiwa vito vya mabilioni akiwa likizoni Paris

153
0
Share:

Mwanadada maarufu kutoka marekani Kim Kardashian ambae pia ni mke wa Rapa maarufu duniani Kanye West amepatwa na misukosuko ya aina yake akiwa katika mapumziko mjini Paris mapema leo

Taarifa kutoka mjini Paris zimesema kuwa mwanadada huyo amevamiwa na watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ambao walivalia mavazi ya askari huku wakiwa wameficha nyuso zao kwa barakoa nyeusi (black masks).

Aidha taarifa kutoka kwa wanausalama wa Paris wamesema kuwa Kim ameibiwa boksi la vito vyenye thamani ya Euro Milioni 5 sawa na dola Milioni 6.7 (£5.2m; $6.7m) ambazo kwa pesa za madafu ni sawa na Bilioni 14.527 pamoja na pete yenye thamani ya Bilioni 9.733799

Msemaji wa mwanadada huyo amesema kuwa Kim alifungiwa bafuni na watu wawili walioficha sura zao wakiwa wameshika bastola, na walimtishia sana japo hawakumuumiza sehemu yoyote ya mwili wake

Kim ambae ni mama wa watoto wawili ameripotiwa kuondoka mjini humo haraka mara tu baada ya kufikwa na mkasa huo.

Aidha taarifa kutoka mjini New York zimesema kuwa Mume wa Kim Kardashian, Kanye West alikuwa stejini akipiga shoo ya aina yake kwenye Tamasha la Muziki na Sanaa la mjini New York wakati alipopewa taarifa za kuvamiwa kwa mke wake na kuamua kuahirisha shoo yake

Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC)

kim-kardashian-Kim Kardashian

Share:

Leave a reply