Kiongozi wa Boko Haram ajeruhiwa vibaya kwenye shambulio la angani

293
0
Share:

Kiongozi wa kikundi cha Kigaidi cha Boko Haram nchini Nigeria, Abubakar Shekau amejeruhiwa vibaya katika shambulio la Angani lililofanywa na jeshi la nchi hiyo huku taarifa za kuumia kwa kiongozi huyo zikitolewa na jeshi la nchini Nigeria huku makamanda wengine wakuu wa kundi hilo wakiuawa.

Shambulio hilo lilitekelezwa siku ya Ijumaa ya Tarehe 19 Agosti wakati viongozi hao walipokuwa wakishiriki sala ya Ijumaa katika kijiji cha Taye eneo la Gombole katika msitu wa Sambaisa jimbo la Bono.

Taarifa kutoka jeshi la Polisi linasema kuwa, makamanda ambao wameuawa ni pamoja na Abubakar Mubi, Malam Nuhu pamoja na Malam Usman waliokuwa na vyeo chini ya Shekau kiongozi mkuu anayeaminika kuwa amejeruhiwa vibaya begani.

Jeshi la polisi limesema kupitia taarifa iliyotolewa na Naibu Mkuu wa mawasiliano Kanal Sani Kukasheka Usman huku kundi hilo la Boko Haram kwa siku za hivi karibuni likiwa limekabiliwa na mzozo wa uongozi ndani yao.

Kikundi cha Islamic State kilitangaza kwamba kwa sasa Abu Musab Al Barnawe ndiye kiongozi mpya wa Boko Haram lakini muda mfupi baadae Shekau alisema kuwa bado ndiye aneyeliongoza kundi hilo na akamshutumu Al Barnawi kwa kujaribu kufanya mapinduzi dhidi yake.

Islamic State ambalo tawi lake la Afrika Magharibi ni Boko Haram walitangaza kupinduliwa kwa kiongozi huyo kutokana na taarifa kusambaa kufariki kwa kiongozi huyo wakiwa na miaka saba tangu walipoanza mashambulizi ya kutaka kuitoa madarakani serikali ya Nigeria na wamesababisha zaidi ya vifo vya watu 20000 hususani katika eneo la kaskazini mashariki.

IS walimtangaza Al Barnawi kuwa kiongozi mpya wa kundi hillo na kusema kuwa nchini ya Shekau ndani ya miezi 18 pekee wamepoteza eneo kubwa walilokuwa wakidhibiti baada ya kukabiliwa vilivyo na jeshi la Nigeria pamoja na majirani zake.

Na Derick Highiness

Share:

Leave a reply