Kituo cha runinga na redio Afghanistan chavamiwa na watu wenye silaha

430
0
Share:

Watu wenye silaha za moto wanadaiwa kuvamia kituo cha redio na runinga ya taifa ya Afghanistan vilivyopo Mashariki mwa nchi hiyo kwenye mji wa Jalalabad.

Taarifa zinaeleza kuwa watu hao walikuwa watatu na ilisikika milio ya risasi ambazo walikuwa wakirushiana na walinzi wa vituo hivyo, risasi zilizosababisha kwa watu sita wakiwemo waandishi wa habari.

Msemaji wa Serikali ya Afghanistan, Attaullah Khughyani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa watu hao walikuwa silaha za moto na kwa sasa bado hawajajua nini hasa chanzo cha tukio hilo na watu hao ni kina nani.

“Tunathibitisha kuwa kuna watu wamevamia katika majengo hayo, kuhusu wao au dhumuni la wao kufanya hivyo bado hatujajua,” alisema Khughyani wakati akifanya mahojiano na kituo cha habari cha Reuters.

 

Share:

Leave a reply