HOT NEWS: Kocha wa zamani wa Nigeria, Stephen Keshi afariki dunia

272
0
Share:

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria na kocha wa zamani wa timu hiyo, Stephen Keshi amefariki dunia alfajiri ya Jumatano ya Juni, 8 akiwa na umri wa miaka 54.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na kaka wa Stephen Keshi, Emmanuel Ado ambae amesema kuwa chanzo cha kifo cha ndugu yake ni mshtuko wa moyo ambao ulimpata baada ya mke wake, Kate Keshi kufariki mwaka jana mwishoni.

“Familia ya Ogbuenyi Fredrick Keshi ya Illah wa Oshimili Kaskazini ya Delta State, tunarudisha shukrani zetu kwa Mungu na tunatangaza kifo cha Mr. Stephen Okechukwu Chinedu Keshi,

“Tangu kifo cha mke wake Mrs. Kate Keshi, Keshi amekuwa katika hali ya maombolezo kwa kipindi chote na alikuwa amepanga kurejea nyumbani Jumatano lakini alipata mshtuko wa moyona akakutwa akiwa ameshapumzika,” alisema taarifa ya Ado.

Aidha Ado ameeleza kuwa familia imebaki katika hali ya huzuni na wanachokifanya kwa sasa ni kumshukuru Mungu na kumwombea apumzike salama.

Kifo cha Keshi kimekuja ikiwa ni miezi sita tangu kufariki kwa mke wake, Kate aliyefariki Disemba, 9 mwaka jana.

Share:

Leave a reply