Kongamano la uwajibikaji kwa wadau wa sekta ya Mafuta na Gesi (Picha)

275
0
Share:

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango afungua Kongamano la uwajibikaji katika sekta ya Mafuta na Gesi lililoandaliwa na taasisi ya WAJIBU – Institute of Public Accountability lililofanyika Aprili 11,2016 jijini Dar es Salaam. Zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali yaliyojiri kwenye kongamano hilo.

Philip Mpango

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango akizungumza na wadau (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Kongamano la uwajibikaji katika sekta ya Mafuta na Gesi lililoandaliwa na taasisi ya WAJIBU – Institute of Public Accountability Aprili 11,2016 jijini Dar es Salaam.

Ludovick Utouh

Mkurugenzi wa Taasisi ya WAJIBU – Institute of Public Accountability Bw. Ludovick Utouh akizungumza na wadau waliyoshiriki Kongamano linalohusu uwajibikaji katika sekta ya Mafuta na Gesi (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi jijini Dar es Salaam.

Philip Mpango

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango (kulia) akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Taasisi ya WAJIBU – Institute of Public Accountability na (kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bw.Ludovick Utouh, sherehe hizo zimefanyika jijini Dar es Salaam.

Gesi na Mafuta

Baadhi ya wadau waliyoshiriki Kongamano linahusu Uwajibikaji katika sekta ya Gesi na Mafuta wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya TWAWEZA Bw.Aidan Eyakuze (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo lililofanyika jijini Dar es Salaam.

PIX 6

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU – Institute of Public Accountability Bw.Ludovick Utouh wakiwa wanaonyesha kibao kinachoonyesha ufunguzi rasmi wa taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam.

Philip Mpango

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wadau waliyoshiriki Kongamano la Uwajibikaji katika sekta ya Mafuta na Gesi,(watatu kulia ni)aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na (watatu kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU – Institute of Public Accountability Bw.Ludovick Utouh.

PIX 5 (B)

Share:

Leave a reply