Korea Kaskazini yaituhumu CIA kupanga njama za kumuua Kim Jong-un

1032
0
Share:

Korea Kaskazini imetuhumu madalali wa Marekani na Korea Kusini kuwa wanapanga njama za kumuua kiongozi wa taifa hilo Kim Jong-un.

Shirika la Habari la Korea Kaskazini (KCNA) limeripoti kuwa njama hiyo inahusisha kutumiwa kwa silaha ya kikemikali pamoja na kemikali yenye miali nururishi na sumu, na kwamba matokeo ya shambulio hilo yataanza kubainika baada ya miezi sita hadi 12.

Taarifa kutoka wizara ya usalama nchini humo, pia inasema kwamba mawakala wa kundi la kigaidi linaloungwa mkono na Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) na Shirika la Ujasusi la Korea Kusini wameingia nchini Korea Kaskazini kufanya mashambulizi wakiwa na silaha hatari za kemikali.

Hata hivyo, taarifa hiyo imesema Korea Kaskazini itawasaka mawakala hao na kuwaangamiza bila huruma. Aidha, Korea Kaskazini imeyasema hayo huku wasiwasi ukiendelea kuongezeka katika rasi ya Korea.

Vita ya maneno kati ya Marekani na Korea Kaskazini imezidi wiki za hivi  karibuni ambapo Korea Kaskazini imetishia kufanya jaribio la sita la silaha za nyuklia.

Share:

Leave a reply