LADY JAYDEE & THE BAND KUANGUSHA BONGE LA SHOW, DODOMA 26 NOVEMBA

470
0
Share:

JUMAMOSI ya  26 Novemba katika mji wa Dodoma kutakuwa na Show moja tu ambayo kwa sasa ni habari ya mjini  ni kutoka kwa Mwanadada mkali, anayetamba kwenye tasnia ya burudani kwa muda mrefu mwanamuziki  Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’.

Lady Jaydee ataangusha bonge la show jukwaani akiwa pamoja na bendi yake iliyojaa vipaji lukuki vya muziki.  Show itafanyika Jumamosi tarehe 26 Novemba ndani ya  ukumbi wa Royal Village Area C na kiingilio kawaida ni Tsh. 10,000,  na V.I.P Tsh. 30,000.

Tayari tiketi za shoo hiyo zimeanza kuuzwa kaatika maeneo mbalimbali ikiwemo ya Dodoma ikiwemo. Pork joint, Ray Kids,Salama Saloon,Royal Village, Mafuru Materephone,.Wakunyamba Classic, Matei Lounge, Chuo cha mipango na Udom.

Hii si ya kukosa, Unataka kumuona shemeji! Basi tukutane pale 26 Nov, Royal Village, shoo ya kistaarabu ndani ya Makao makuu ya nchi..unakosaje sasa!!!!

Lady Jaydee

Ladyjaydee “Sawa na wao”

 

Share:

Leave a reply