Letshego yasaidia kuboresha miundombinu ya maji katika makazi ya wazee

192
0
Share:

Katika kuadhimisha miaka 18 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere jumuiya ya
wafanyakazi wa taasisi ya fedha ya Letshego Tanzania wameadhimisha siku hiyo kwa kutembelea
makazi ya wazee wasiojiweza na walemavu Nunge, Kigamboni.

Wafanyakazi hao walipata nafasi ya kusikiliza mahitaji ya wazee hao na katika jitihada za kutatua baadhi ya changamoto za wakazi wa Nunge kwa siku hiyo walitoa msaada wa tenki moja la maji la ujazo wa lita 7000 ikiwa ni pamoja na kulipia gharama zote za ufungwaji na uunganishaji wa mabomba katika tenki hilo na kukabidhi risiti ya malipo ya umeme luku kiasi cha cha shillingi 500,000 kwa Mkuu wa Kituo cha Nunge, Ojuku Mgedzi.

Aidha Mkurugenzi wa Letshego Tanzania, Yohane Kaduma aliahidi kutoa pampu kubwa ya
maji kwa kituo cha Nunge ambayo itasaidia kulimaliza kabisa tatizo la usambazaji wa maji katika
kambi hiyo.

Share:

Leave a reply