Licha ya matokeo yasiyowafurahisha mashabiki, huu ndiyo msimamo wa uongozi wa Man United

700
0
Share:

Matarajio ya mashabiki wengi wa klabu inayoongoza duniani kwa kuwa na mashibiki wengi, Manchester United ya kuona timu yao ikipata matokeo mazuri kwa msimu wa 2016/2017 baada ya kocha Jose Mourinho kukabidhiwa mikoba ya kuinoa klabu hiyo yamekuwa tofauti.

Kwani katika michezo 14 ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) ambayo imeshacheza mpaka sasa, Man United imepata ushindi katika michezo mitano pekee, ikitoa sare michezo sita na kufungwa mitatu.

Matokeo hayo yamekuwa yakiwashangaza mashabiki wengi kwa kuona hali inakuwa tofauti na matarajio yao na hata baadhi wakianza kumtolea maneno kocha Mourinho ambaye awali alikuwa akifundisha Chelsea ambapo alitimuliwa kazi kutokana na kupata matokeo mabaya.

Lakini hali ni tofauti kwa uongozi wa Man United, kwani unaonyesha imani kwa Mourinho na unaamini hali itakuwa nzuri na timu itaanza kupata matokeo kwani inawachezaji wenye uwezo mkubwa na ambao wanaweza kuisaidia timu kushinda katika michezo ya mashindano mbalimbali ambayo inashiriki.

Akizungumza na mtandao wa ESPNFC, mmoja wa watu ambao yupo karibu na uongozi wa Manchester United alisema uongozi unamkubali Mourinho kwani uwezo wa klabu umeongezeka tofauti na msimu uliopita na kwao si kupata matokeo tu ila kuweka msingi bora ambao utatumika kwa muda mrefu.

Share:

Leave a reply