Listi ya Mabilionea 21 wa Afrika, MO Dewji aongoza Afrika Mashariki na Kati

3250
0
Share:

Jarida la Forbes la Marekani limetoa orodha ya Mabilione 21 waliopo katika bara la Afrika ambapo Mnigeria, Aliko Dangote ameendelea kushika nafasi ya kwanza licha ya utajiri wake kupungua kwa asilimia 27.9% akiwa na utajiri wa Dola Bilioni 12.7.


Nafasi ya pili imeshikwa na mfanyabiashara kutoka Afrika Kusini, Nicky Oppernheimer akiwa na utajiri wa Dola Bilioni 7 na nafasi ya tatu ikishikwa na Mike Adenuga kutoka Nigeria ameshika nafasi ya tatu akiwa na utajiri wa Dola Bilioni 5.8.

Katika listi hiyo, Tanzania pia imetajwa kupitia Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji kushika nafasi ya 17 akiwa sawa na Aziz Akhannouch wa Morocco ambao wote wana utajiri unaokadiriwa kufikia Dola Bilioni 1.4.

Pia Mohammed Dewji amesalia kuwa bilionea mdogo Afrika akiwa na miaka 41 na nafasi ya pili ikishikwa na Isabel dos Santos kutoka Angola ambaye ana miaka 43 na Stephen Saad wa Afrika Kusini akishika nafasi ya tatu akiwa na miaka 52.

JINA UTAJIRI TAIFA
1.    Aliko Dangote Dola Bilioni 12.1 Nigeria
2. Nicky Oppernheimer Dola Bilioni 7 Afrika Kusini
3. Mike Adenuga Dola Bilioni 5.8 Nigeria
4. Johann Rupert Dola Bilioni 5.5 Afrika Kusini
5. Christoffel Wiese Dola Bilioni 5.5 Afrika Kusini
6. Nassef Sawiris Dola Bilioni 5.3 Misri
7. Naguib Sawiris Dola Bilioni 3.7 Misri
8. Isabel dos Santos Dola Bilioni 3.2 Angola
9. Issad Rebrab Dola Bilioni 3.1 Algeria
10. Mohamed Mansour Dola Bilioni 2.7 Misri
11. Koos Bekker Dola Bilioni 2 Afrika Kusini
12. Othman Benjelloun Dola Bilioni 1.9 Morocco
13. Yasseen Mansour Dola Bilioni 1.8 Misri
14. Folorunsho Alakija Dola Bilioni 1.6 Nigeria
15. Patrice Motsepe Dola Bilioni 1.6 Afrika Kusini
16. Aziz Akhannouch Dola Bilioni 1.4 Morocco
17. Mohammed Dewji Dola Bilioni 1.4 Tanzania
18. Youssef Mansour Dola Bilioni 1.1 Misri
19. Onsi Sawiris Dola Bilioni 1.1 Misri
20. Anas Sefrioul Dola Bilioni 1.1 Morocco
21Stephen Saad Dola Bilioni 1.1 Afrika Kusini
Share:

Leave a reply