Listi ya mikoa tisa inayoongoza kwa uchache wa watumishi wa sekta ya afya

470
0
Share:

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameitaja mikoa tisa ambayo inaongoza kwa kuwa na idadi ndogo ya watumishi wa afya jambo ambalo linasababisha baadhi ya huduma kutotolewa kwa wakati kutokana na uwepo wa watumishi wachache.

Akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, waziri Ummy ameitaja mikoa hiyo kuwa ni Kigoma, Katavi, Geita, Simiyu, Shinyanga, Kagera, Rukwa, Tabora na Singida.

Waziri Ummy alisema kutokana na kuwepo upungufu huo Serikali imepanga kuipa kipaumbele mikoa hiyo pindi itakapotangaza nafasi za kazi ili na yenyewe ipate watumishi ambao watapelekwa katika hospitali na vituo vya afya.

“Leo nimetembea wilaya ya Mpanda na Tanganyika (Mpanda V) kufuatilia utoaji wa huduma za afya, Changamoto kubwa ni watumishi, ajira mpya za watumishi wa afya tutatoa kipaumbele kwa mkoa wa Katavi na mikoa mingine 8 yenye uhaba mkubwa,” alisema waziri Ummy.

Share:

Leave a reply