Liverpool, Roma zatinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

114
0
Share:

Klabu ya Liverool ya Uingereza na AS Roma ya Italia zimefanikiwa kuingia katika nafasi ya nsu fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kwa kuitoa Manchester City ya Uingereza na Barcelona ya Hispania.

Liverpool imewaondoa Man City kwa ushindi wa jumla wa goli 5-1 ambapo katika mchezo wa kwanza uliopikwa katika dimba la Anfield, Liverpool iliibuka na ushindi wa goli 3-0 na katika mchezo wa marudiano uliopigwa katika dimba la Etihad, Liverpool ikaibuka tena na ushindi wa 2-1.

Kwa upande wa AS Roma imewaondoa Barcelona kwa sheria ya goli la ugenini baada ya matokeo ya jumla kuwa goli 4-4. Katika mchezo wa kwanza uliopigwa katika dimba la Camp Nou, Barcelona iliibuka na ushindi wa goli 4-1 lakini katika mchezo wa marudiano uliopigwa Italia katika dimba Stadio Olimpico, Roma imeibuka na ushindi wa goli 3-0 na hivyo kuiondoa Barcelona.

Michezo mingine ya marudiano ya robo fainali ya ligi hiyo inataraji kupigwa leo jumatano Aprili, 11 ambapo Real Madrid itakuwa mwenyeji wa Juventus na Bayern Munich ikiwakaribisha Sevilla.

Katika michezo ya kwanza, Real Madrid iliibuka na ushindi wa goli 3-0 na Bayern Munich iliibuka na ushindi w agoli 2-1.

Share:

Leave a reply