Liverpool yatinga nusu fainali ya Europe League, yaipiga 4-3 Dortmund

250
0
Share:

Michezo ya robo fainali ya Ligi ya Vilabu barani Ulaya (Europe League) imeendelea usiku wa Alhamisi kwa michezo minne ambapo Liverpool ilikuwa mwenyeji wa Dortmund katika uwanja wa Anfield na Liverpool kuibuka na ushindi wa goli 4-3.

Magoli ya Liverpool yalifungwa na Divock Origi dk. 48, Philippe Coutinho dk. 75, Mamadou Sakhp dk. 78 na Dejan Lovren katika dakika ya 90 huku magoli ya Dortmund yakifungwa na Henrik Mkhitaryan dk. 5, Pierre-Emerick Aubameyang dk. 9 na Mats Hummels akiwa dakika ya 53.

Matokeo ya michezo mingine ni;

Sevilla 1 – 2 Athletic Bilbao

Shakhtar Donetsk 4 – 0 Braga

Sparta Prague 2 – 4 Villarreal

Baada ya matokeo hayo Liverpool, Sevilla, Shakhtar Donetsk na Villarreal zimefuzu hatua ya nusu fainali ya Kombe la Ligi ya Vilabu barani Ulaya (Europe League).

Share:

Leave a reply