Lori lapitishwa makusudi mtaa wa soko na kuua 12

374
0
Share:

WATU 12 wamekufa na wengine 48 kujeruhiwa wakati lori lilipopitishwa kwa makusudi katika mtaa wa soko wenye watu wengi kwenye gulio la Krismasi katikati ya jiji la Berlin, nchini Ujerumani.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani, Thomas de Maiziere, amekataa kusema kama hilo ni shambulio la kigaidi au ingawa viashiria vingi vinaonesha ni shambulio la kukusudia.

Polisi wamesema kwamba dereva wa lori hilo amekamatwa na sasa anahojiwa.

Aidha imeelezwa abiria mmoja katika lori hilo naye alikufa kutokana na majeraha aliyoyapata.

Gulio hilo lipo Breitscheidplatz, karibu na Kurfuerstendamm, mtaa muhimu wa masoko, magharibi mwa jiji la Berlin.

Imeelezwa kuwa takaribani watu 50 wapo hospitali na wanne wapo katika uangalizi maalumu.

Watu wa usalama wamesema kwamba dereva wa lori hilo alikuwa ni mkimbizi aliyetafuta hifadhi akitokea Afghanistan au Pakistan Februari mwaka huu.

christmas-market-in-belin

Msemaji wa Polisi Jijini Berlin , Winfried Wenzel amesema kwamba mtu aliyetuhumiw akuendesha lori hilo alidakwa kiasi cha kilomita 2 toka eneo la maafa karibu na Mnara wa Victory Column.

Namba za gari zinaonesha kwamba lori hilo limesajiliwa nchini Poland na Polisi wanaamini kwamba lklikuwa limeibwa.

Polisi wanasema kwamba abiria aliyekufa ni Mpoland.

Mmliki wa lori hilo Ariel Zurawski, amethibitisha kwamba dereva wa lori hilo amepotea na hawajui aliko.

Je ni shambulio la kigaidi?

Wanasiasa wa Ujerumani hawako tayari kusema kama hilo ni shambulio la kigaidi huku mambo mengi yakiwa hayako wazi.

Waziri wa mambo ya ndani de Maiziere ameiambia televisheni ya ARD  kwamba ni mapema sana kusema kwamba hilo lilikuwa shambulio la kigaidi ingawa viashiria vingi vinaelekeza hivyo.

Anasema kwamba  pamoja na viashiria hivyo kuwapo, wanasubiri uchunguzi ufanyiek kwanza na kuwa na uhakika hilo ni tukiola aina gani kabla ya kulitaja.

Kiongozi wa Ujerumani , Kansela Angela Merkel  ameambiwa tukio hilo na Waziri wa Mambo ya ndani huku Meya wa Berlin kupitia msemaji wake Steffen Seibert  akisema kwamba wanaomboleza wale waliokufa na kuomba waliojeruhiwa kupata msaada na kupona haraka.

Lorry Drives Through Christmas Market In Berlin

Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck amesema kwamba Jumatatu  ilikuwa siku mbaya kwa Berlin na taifa hilo la Ujerumani.

Imeelezwa kuwa lori hilo ghafla lilibadili mwelekeo na kuvamia mtaa huo  ambao ulikuwa umejaa watu wakifanya shughuli mbalimbali na kupamia vibanda vya mbao ambavyo vilikuwa vimejaa wateja na watalii mbalimbali.

Inaaminika kwamba lori hilo lilifanikiwa kuvuruga kiasi cha mita 50-80 kabla halijasimama.

Shambulio la Ujerumani limerejesha kumbukumbu ya shambulio la Nice Ufaransa Julai 14 ambapo shambulio la lori liliua watu 86.

Shambulio hilo lilidaiwa kufanywa na mmoja wa wahanga kutoka IS.

Taasisi za kigaidi za IS na al-Qaida zimekuwa zikiwataka wafuasi wake kutumia malori kama silaha za kushambulia maeneo yenye watu wengi.

Share:

Leave a reply