Ma Dj wa ‘Sauzi’ Waufagilia muziki wa Bongo

702
0
Share:

Wachezesha muziki ‘ma DJ’ maarufu Afrika Kusini Siyabonga Sibeko ‘DJ Capital’ na Lutendo Kungoane ‘Dj Sliqe’ wamesema  kwa sasa muziki wa Tanzania upo vizuri na utafika mbali.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari katika hoteli ya New Africa, Dar es Salaam ma DJ wa Redio na Telesheni Afrika Kusini walisema kwa sasa Tanzania imepiga hatua kubwa kimuziki.

“Kwa sasa huwezi kuzungumzia nchi zinazofanya vizuri kwa kiwango cha juu kimuziki Afrika bila kuitaja Tanzanja,”alisema Dj Capital na kuongeza “Afrika Kusini, Nigeria, Ghana, Tanzania na Kenya hizo ndizo nchi za Afrika zinazofanya vizuri katika muziki wa kisasa,”alisema.

Kwa upande wake DJ Sliqe’ alisema kwamba anavutiwa zaidi na wasanii wawili wa Tanzania kwa sasa, ambao ni Diamond Platnumz na Vanessa Mdee.

“Ni wasanii wengi wa Tanzania wanaofanya vizuri kwa sasa, lakini mimi upande wangu nawapenda zaidi hao wawili,”alisema.

Wawili hao, wote ni Ma DJ wa kituo cha Redio cha Touch Central cha Johannesburg, Afrika Kusini wakati DJ Capital pia anafanya kipindi cha Club 808 cha Televisheni ya ETV nchini humo.

Wawili ambao wamekuja nchini kwa ziara ya wiki moja kujifunza zaidi kuhusu muziki wa Tanzania, pia ni Ma DJ wa kumbi za disko nchin kwao.

“Tumekuja hapa kujigunza na kukutana na wasnaii kwa sababu sisi pia ni watayarishaji wa muziki,”alisema Capital.

Wapiga muziki ‘ma DJ’ maarufu Afrika Kusini Siyabonga Sibeko ‘DJ Capital’ na  Lutendo Kungoane ‘Dj Sliqe’  wakizungumza na waanadishi wa habari ( hawapo pichani), Dar es Salaam kuhusiana na ziara yao ya wiki moja nchini katika kujifunza vitu tofauti kimuziki.

Wapiga muziki ‘ma DJ’ maarufu Afrika Kusini Siyabonga Sibeko ‘DJ Capital’ na  Lutendo Kungoane ‘Dj Sliqe’  wakiwa katika pozi

Share:

Leave a reply