Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kupata taarifa kufanyika Septemba 28

220
0
Share:

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya kupata taarifa inatarajia kufanyika Septemba 28, mwaka huu ambapo wadau wa habari wameiomba Serikali  kutekeleza sheria ya kupata taarifa.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari mapema leo,  Mwenyekiti wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa, Kajubi Mukajanga amesema Serikali na wadau wanao wajibu wa kutekeleza sheria hiyo ilikutoa fursa na haki ya kupata taarifa.

 

Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja Utetezi toka taasisi ya Twaweza Bi. Annastazia Rugaba wakati akielezea hali ya upatikanaji wa taarifa Serikalini kuelekea maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kupata taarifa Septemba 28.

Meneja Utetezi toka taasisi ya Twaweza Bi. Annastazia Rugaba akielezea kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) hali ya upatikanaji wa taarifa Serikalini kuelekea maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kupata taarifa Septemba 28.

Meneja Utetezi toka taasisi ya Twaweza Bi. Annastazia Rugaba akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akiiomba Serikali kutekeleza sheria ya kupata taarifa kuelekea maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kupata taarifa Septemba 28, katikati ni Mwenyekiti wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa Kajubi Mukajanga na kushoto ni Meneja Programu wa Baraza la Habari Tanzania(MCT) Bi. Pili Mtambalike

 

Mwenyekiti wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa, Kajubi Mukajanga (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kupata taarifa Septemba 28 na kuiomba Serikali kutekeleza sheria ya kupata taarifa, katikati ni Meneja Utetezi toka taasisi ya Twaweza Bi. Annastazia Rugaba na kushoto ni Meneja Programu wa Baraza la Habari Tanzania(MCT) Bi. Pili Mtambalike.

Picha na Eliphace Marwa – Maelezo.

Share:

Leave a reply