Maalim Seif aanza ziara rasmi Bara

504
0
Share:

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad leo Mei 1,2017 ameanza ziara rasmi ya siku tatu katika wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam na kuwataka wanachama wa chama hicho kujiandaa kwenda kuchukua ofisi yao ya Buguruni wakati wowote kuanzia sasa.

Aidha, Maalim Seif amewahakikishia wanachama na wananchi waliojitokeza, kuwa CUF ni taasisi imara na kwamba haiwezi kuyumbishwa bali itazishinda changamoto zote zinazojitokeza.

Baada ya ziara ya mkoa wa Dar es Salaam kumalizika, Maalim Seif ataanza ziara rasmi ya ukaguzi wa uhai na shughuli za Chama hicho katika Mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.

Katika msafara huo Maalim Seif aliambatana na Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Musa Kafana, Naibu Meya wa Ilala Omari Kumbilamoto, na Mbunge wa Temeke  Abdallah Mtolea ambaye pia  Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa, Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uchaguzi Shaweji Mketo pamoja na viongozi wengine mbalimbali wa Jumuiya za Chama na Walinzi (Blue Guards).

Na Regina Mkonde

Share:

Leave a reply