Maaskofu watakiwa kupeleka hoja zao Bungeni

293
0
Share:

Baada ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa la KKKT kutoa Waraka wenye ujumbe kwa serikali, Mbunge wa Viti Maalumu wa CUF, Riziki Rulida amewataka maaskofu hao kupeleka hoja za malalamiko yao Bungeni kwa ajili ya kupata ufumbuzi badala ya kutumia majukwaa ya dini.

Rulida amesema hayo leo Aprili 5, 2018 Bungeni mjini Dodoma ambapo ameitaka serikali kulisimamia kikamilifu suala hilo, kwa madai kuwa ujumbe wa waraka huo unaweza kushawishi vijana kuingia mitaani na kuhatarisha amani ya nchi. 

“Viongozi watangaze dini, uadilifu na amani kwa waumini wao, wanataka kuleta mchezo wa propaganda kuingiza kwenye dini haikubaliki. Tanzania tunahitaji amani na amani haichezewi, watu wanajaribu kuangalia ubinafsi bila kuangali nchi inaelekea wapi, panapotokea vita wahanga ni wanawake na watoto, wahenga wanasema usipojenga hufa hutajenga ukuta, lakini mwanzo choko choko ndogo zinazoanza iwe za kidini au za kisiasa,” amesema na kuongeza.

“Serikali isimamie kikamilifu kwa mfano mimi hapa mlemavu ikianza vita mtakimbia wote mtaniacha mimi, wagonjwa wazee watakuwa wahanga wa vita, watanzania hatutaki vita, kama kuna hoja walete hoja itafutwe ufumbuzi na usuluhishi kutumia majukwa ya dini kutangaza mazungumzo yatakayowapa vijana mheko wa kuingia mitaani haikubaliki.”

Share:

Leave a reply