Mabalozi wa Usalama barabarani ‘RSA’ kufanya kampeni ya “Abiria paza sauti” kila Jumamosi

321
0
Share:

Asasi ya kiraia ya Road Safety Ambassadors (RSA) leo Desemba 2,2017 imeanza rasmi kampeni yake ya Abiria paza sauti katika kipindi hiki ambacho tunaelekea kumaliza mwaka 2017 ikiwa na lengo la kutokomeza ajari ambazo zimekuwa zikijitokeza mwisho wa mwaka.

Kupitia taarifa yao ya ukurasa wa facebook  wa mabalozi hao, wameeleza kuwa:

“Ndugu Mabalozi, Karibuni sana tushiriki pamoja katika kampeni ya abiria paza sauti ambayo itafanyika nchi nzima kuanzia tarehe 02.12.2017. Katika kampeni hiyo tutaelimisha na kuhamasisha umma kuhusu usalama barabarani na kujifunza mambo mbalimbali.

 Kampeni itaendeshwa zaidi katika vituo vya mabasi. Kila balozi apate kushiriki mkoani kwake. SOTE TUSEME, HATUTAKI AJALI MWEZI WA 12. ACCIDENT FREE DECEMBER.” Ulieleza ujumbe huo.

RSA imekuwa ikiendesha kampeni hiyo yenye lengo la kuweza kusaidia kutokomeza ajari ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara kila ifikipo mwisho wa mwaka kutokana na watu wengi kuwa wakirudi nyumbani kusherekea sikukuu za kufunga mwaka pamoja na familia zao.

Kampeni hiyo ambayo inaanza leo, inatarajiwa kufanyika kila Jumamosi nchi nzima yaani leo Desemba 2, Desemba 9, Desemba 16,na Desemba 23 mwaka huu.

Hadi sasa  kwa upande wa SUMATRA wameweza kuweka namba maalum ambazo abiria anaweza kuzitumia endapo ataona dereva anakwenda mwendo wa hatari ama vingine katika makosa ya barabarabi kwa kupiga kutoa taarifa pindi waonapo viashiria hivyo kuwa ni 0800110019 na 0800110002 ambapo namba hizo zinapatikana masaa 24 na gharama za kupiga simu ni bure.

 

Share:

Leave a reply