Mabasi ya uokoaji nchini Syria yawasili salama katika mji wa Aleppo

282
0
Share:

Msafara wa takribani mabasi kumi yaliobeba manusurika kutoka katika mji cha Shiite Muslim katika vijiji vya Foua na Kefraya ambao walikwama kati kati ya mapigano na kuzuiliwa kwa miaka na waasi wa Syria waliwasili katika mji wa Aleppo leo Jumatatu, Televisheni ya taifa ya Syria imesema.

Uokoaji wa raia kutoka katika vijiji hivyo ulikuwa katika wakati mgumu pale wiki iliyopita waasi waliopoanza kuwashambulia raia waliokuwa wakiokolewa lakini maelfu ya raia waliweza kuondolewa katika vijiji hivyo vilivyokuwa chini ya waasi kwa miaka kadhaa ya mapigano makali.

Share:

Leave a reply