Macron atishia kuishambulia Syria

102
0
Share:

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametishia kuishambulia Syria endapo ushahidi utabainika kwamba serikali yake inatumia silaha za kemikali dhidi ya raia. 

Macron aliwaambia wanahabari kuwa, atashambulia maeneo ambayo silaha hizo hutengenezwa au inapofanyika mipango ya utengenezaji wa silaha hizo.

Hata hivyo, Macron amekiri kuwa, hadi sasa bado uchunguzi haujaonyesha kama silaha zilizopigwa marufuku zimetumiwa. 

Tamko lake hilo limekuja siku kadhaa baada ya kutokea mashambulizi ya kutumia silaha za Chlorine nchini Syria tangu mwezi Januari mwaka huu.

Share:

Leave a reply